

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China atoa wito kwa China, Japan na Korea Kusini kukataa uingiliaji kutoka nje
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akizungumza kwenye mkutano wa nane wa kibiashara kati ya China, Japan na Korea Kusini, mjini Seoul, Jamhuri ya Korea, Mei 27, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)
SEOUL - Waziri Mkuu wa China Li Qiang siku ya Jumatatu alipohudhuria mkutano wa nane wa kibiashara kati ya China, Japan na Korea Kusini pamoja na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema kwamba China, Japan na Korea Kusini zinapaswa kujitahidi kukataa uingiliaji kutoka nje na kuendelea kuwa na dhamira ya kuishi pamoja kwa masikilizano na kuungana mkono.
Rais Xi Jinping wa China anatumia kanuni ya upendo, udhati, kunufaishana na ujumuishaji ili kujumuisha kwa ufupi diplomasia ya ujirani mwema ya China, Li amesema huku akiongeza kuwa China, Japan na Korea Kusini, ambazo kijiografia zimetenganishwa na ukanda mwembamba wa maji, zinapaswa kuwa majirani wenye amani na urafiki.
Li amezitaka pande hizo tatu kujifunza kutoka kwenye historia na kutazama mustakabali wa siku za baadaye, kuendana na matakwa ya watu wa nchi hizo tatu ya kuishi na kufanya kazi kwa amani, kujitahidi kuondoa uingiliaji kutoka nje, na daima kuishi kwa maelewano na kudumisha mshikamano.
Ushirikiano wa kina wa kiuchumi kati ya China, Japan na Korea Kusini unaamua kwamba nchi hizo tatu zinapaswa kuwa majirani wa karibu kwa kujiendeleza kwa pamoja, kuchukuliana kama washirika wa karibu na fursa muhimu katika njia za kujiendeleza, kuendelea kutafuta faida za kifursa zinazoendana pamoja na maeneo ya ukuaji wa ushirikiano wa uchumi wa nchi hizo tatu ili kufikia kiwango cha juu cha kunufaishana kwa pande zote, Li amesema.
Zikiwa na utamaduni unaofanana, China, Japan na Korea Kusini zinapaswa kuwa majirani wa karibu wanaoelewana, amesema, huku akitoa wito kwa pande hizo tatu kutumia vyema mshikamano wa kitamaduni ili kuhimiza maelewano, imani na ushirikiano wa karibu.
China inapenda kushirikiana na Korea Kusini na Japan ili kuzidisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, kuendelea kuhimiza muunganisho wa maslahi, mshikamano wa pamoja kati ya watu na mustakabali wa pamoja, kuharakisha mafungamano ya kikanda, na kufungua matarajio mapya ya amani, utulivu, maendeleo na ustawi, amesema.
Wawakilishi takriban 240 wa kampuni na serikali kutoka nchi hizo tatu walihudhuria mkutano huo.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akizungumza kwenye mkutano wa nane wa kibiashara kati ya China, Japan na Korea Kusini, mjini Seoul, Jamhuri ya Korea, Mei 27, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma