

Lugha Nyingine
Dhamira ya Jumuiya ya Kimataifa kwa kanuni ya kuwepo kwa China moja ni isiyotetereka: Msemaji wa China Bara
BEIJING – Mkutano wa Baraza la Afya Duniani (WHA) kukataa kile kinachoitwa pendekezo kuhusu Taiwan kwa mara nyingine tena umethibitisha kwamba dhamira ya jumuiya ya kimataifa kwa kanuni ya kuwepo kwa China moja isipinduka, amesema Chen Binhua msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China siku ya Jumatatu.
Chen, ametoa kauli hiyo kuhusu uamuzi wa Kamati Kuu na Mkutano wa Wajumbe Wote wa baraza la 77 la Afya Duniani wa kutojumuisha kile kinachoitwa pendekezo la "kuialika Taiwan kushiriki kwenye WHA kama mwangalizi" lililowasilishwa na baadhi ya nchi katika ajenda yake siku ya Jumatatu. Huu umekuwa mwaka wa nane mfululizo kwa WHA kukataa pendekezo la namna hiyo.
Kuna China moja tu duniani, na Taiwan ni sehemu ya China, Chen amesema.
Amesema, kukataliwa kwa pendekezo hilo pia kunathibitisha kwamba jaribio la mamlaka ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo cha Taiwan la kutegemea vikundi vya nje kushiriki katika WHA bila kutambua Makubaliano ya 1992 ambayo yanajumuisha kanuni ya kuwepo kwa China moja halitafanikiwa.
"Tuna undugu wa damu na watu wa Taiwan, na tunafuatilia afya na ustawi wao siku zote," msemaji huyo amesema.
China Bara itaendelea kuchukua hatua madhubuti, ikiwa ni pamoja na kupanga wataalam wa kiufundi wa matibabu kutoka Taiwan kushiriki katika shughuli za kiufundi za Shirika la Afya Duniani (WHO) na kuijulisha Taiwan juu ya matukio ya dharura ya afya ya umma zinazotolewa na WHO kwa wakati, ili kulinda afya za watu wa Taiwan, Chen alisema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma