Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC yathibitisha sera na hatua za kuharakisha maendeleo ya maeneo ya kati ya China na masharti ya kupunguza hatari za mambo ya fedha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 28, 2024

BEIJING - Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) siku ya Jumatatu imefanya mkutano na kujadili kuhusu sera na hatua za kuharakisha maendeleo ya maeneo ya kati ya China katika zama mpya, na kanuni za majaribio kuhusu kuwajibisha kazi ya kuzuia au kupunguza hatari za mambo ya fedha.

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, aliongoza mkutano huo wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.

Mkutano huo umehimiza juhudi za kupata mafanikio makubwa mapya katika kuharakisha maendeleo ya maeneo ya kati ya China ya mikoa ya Shanxi, Anhui, Jiangxi, Henan, Hubei na Hunan.

Maeneo hayo yanachukua sehemu ya kumi ya ardhi ya China na takriban robo moja ya wakazi wake, yakiwa vituo muhimu vya uzalishaji wa nafaka, nishati na raslimali, uzalishaji wa vifaa vya kisasa na viwanda vya teknolojia za hali ya juu, na pia ni vituo vya usafirishaji na uchukuzi wa bidhaa kwa pande zote.

Mkutano huo umehimiza kushikilia kupata maendeleo kwa kutegemea uvumbuzi na kuimarisha utafiti asilia wa kisayansi na kiteknolojia ili kupata mafanikio mapya.

Juhudi lazima zifanyike ili kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora kulingana na hali halisi ya eneo husika, kuharakisha ujenzi wa mfumo wa kisasa wa viwanda, kuhimiza maendeleo ya sekta ya uchumi halisi na kuongeza nguvu ya ushindani, na kuratibu juhudi katika kuhimiza uboreshaji wa viwanda vya jadi huku kukiwa na kukuza viwanda vinavyoibukia na viwanda vya siku za baadaye.

Mkutano huo umesisitiza juhudi za kuunda mfumo wa kisasa wa miundombinu ya mawasiliano, na kuhimiza mzunguko mzuri, huria na bila vizuizi wa mambo muhimu ya uzalishaji.

Pia umehimiza kazi ya kusukuma mbele uhifadhi wa ikolojia na ulinzi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache.

Mkutano huo umebainisha kuwa kuzuia na kupunguza hatari za mambo ya fedha ni changamoto kubwa inayopaswa kutatuliwa ili kupata maendeleo yenye sifa bora, kwani inahusu usalama wa nchi, mambo ya jumla ya maendeleo, na usalama wa mali za wananchi.

Mkutano huo umesisitiza kuwa kanuni za majaribio za kuzuia na kupunguza hatari za mambo ya fedha zinapaswa kutekelezwa kwa uthabiti ili kutoa ishara kali kwamba mkiukaji yeyote atawajibishwa, ili usimamizi wa mambo ya fedha uwe na "meno na miiba" na kuwa mkali kwa kweli.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha