Mkoa wa Gaza wa Msumbiji warejesha uzalishaji wa ngano kupitia uungaji mkono wa kiteknolojia wa China

(CRI Online) Mei 28, 2024

Jimbo la Gaza, kusini mwa Msumbiji unatarajiwa kurejesha uzalishaji wa zao la ngano katika robo hii ya mwaka, likisaidiwa na teknolojia ya China kupitia kampuni inayowekezwa kwa mtaji wa China.

Kikimnukuu gavana wa jimbo hilo Margarida Chongo, kituo cha Redio cha Msumbiji kimesema, upandaji wa kwanza wa zao hilo unapangwa kuanza ndani ya siku kadhaa katika Eneo la Umwagiliaji maji la Lower Limpopo huko Xai-Xai, mji mkuu wa Jimbo la Gaza.

Gavana huyo amesema, katika kipindi cha kwanza, hekta zaidi ya 150 za shamba zitalimwa ngano. Urejeshaji wa uzalishaji wa ngano katika mfumo wa umwagiliaji wa maji wa Lower Limpopo umetimizwa baada ya karibu miaka 50 kupitia ushirikiano wa teknolojia ya China iliyotolewa na kampuni ya Wanbao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha