

Lugha Nyingine
Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China na Mke wa Rais wa Guinea ya Ikweta waongea na kunywa chai Beijing
Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping na Constancia Mangue de Obiang, Mke wa Rais wa Guinea ya Ikweta wanaongea huku wakikunywa chai mjini Beijing, China, Mei 28, 2024. (Xinhua/Ding Lin)
BEIJING - Siku ya Jumanne, Peng Liyuan, Mke wa Rais wa China Xi Jinping, aliongea na Mke wa Rais wa Guinea ya Ikweta Constancia Mangue de Obiang huku wakikunywa chai mjini Beijing. Bibi Constancia ameambatana na Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Jamhuri ya Equatorial Guinea katika ziara yake ya kiserikali nchini China.
Peng amesema, China na Guinea ya Ikweta ni marafiki na washirika wazuri wanaosaidiana, tunatumai pande zetu mbili zitafanya mawasiliano na ushirikiano zaidi, kulinda na kuhimiza kwa pamoja haki na maslahi ya wanawake, na kufanya juhudi kwa pamoja katika kuinua kiwango cha elimu na afya ya umma ili kuleta manufaa kwa watu wa pande hizo mbili.
Kwa upande wake Constancia ameipongeza China, hususan kwa Peng kujali kwa muda mrefu wanawake na watoto katika nchi za Afrika, ikiwa ni pamoja na Guinea ya Ikweta, na kutoa mchango wa kuimarisha afya na ustawi wao. Bibi Constancia anatarajia kuimarishwa zaidi kwa mawasiliano na ushirikiano na China na kuongezwa kwa urafiki kati ya nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma