

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na mwenzake wa Sudan mjini Beijing
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na mwenzake wa Sudan Hussein Awad, ambaye yuko ziarani nchini China kwa ajili ya mkutano wa 10 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu, mjini Beijing, China, Mei 28, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na mwenzake wa Sudan Hussein Awad, ambaye yuko nchini China kuhudhuria mkutano wa 10 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu ambapo Wang amesema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 65 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, China ina nia thabiti ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati yake na Sudan.
Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema China inaiunga mkono Sudan katika kulinda mamlaka ya taifa, uhuru na ukamlifu wa ardhi yake, kupata amani na utulivu wa ndani, na kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali yake halisi ya taifa.
"China itaendelea kuhimiza jumuiya ya kimataifa kutoa mazingira mazuri ya nje kwa ajili ya kutatua suala la Sudan," amesema Wang kwenye mkutano wao uliofanyika Jumanne mjini Beijing.
Amesema China inathamini uungaji mkono wa dhati wa Sudan na ushiriki wake katika Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu, na kusema China inapenda kutumia mkutano huo wa 10 wa mawaziri kama fursa ya kukuza uhusiano kati ya China na Nchi za Kiarabu.
Wang amesema China pia inapenda kushirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Sudan ili kuandaa kwa mafanikio Mkutano wa kilele wa mwaka huu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ili kutoa mchango katika kujenga jumuiya ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Hussein amepongeza mafanikio makubwa ya China katika maendeleo, na kuishukuru China kwa uungaji mkono wake mkubwa katika maendeleo ya Sudan.
Ameongeza kuwa, Sudan inafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, na daima itaiunga mkono China kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya kimsingi na mambo yanayofuatiliwa na China.
Hussein amesema Sudan inatilia maanani sana Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu na FOCAC, na inapenda kuzidisha ushirikiano wenye matokeo halisi na China katika sekta mbalimbali ndani ya mfumo wa majukwaa hayo mawili muhimu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na mwenzake wa Sudan Hussein Awad, ambaye yuko nchini China kuhudhuria mkutano wa 10 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu, mjini Beijing, China, Mei 28, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma