

Lugha Nyingine
Wafanyakazi wa taaluma katika Chuo Kikuu cha California, Marekani wagoma juu ya namna chuo hicho kilivyoshughulikia maandamano ya wafuasi wa Palestina
![]() |
Wafanyakazi wa taaluma wakiandamana katika Chuo Kikuu cha California (UC), Los Angeles, California, Marekani, Mei 28, 2024. (Picha na Zeng Hui/Xinhua) |
LOS ANGELES - Wafanyakazi wa taaluma katika Chuo Kikuu cha California (UC), Los Angeles, katika Jimbo la California nchini Marekani, wamegoma kufanya kazi siku ya Jumanne wakipinga mfumo wa chuo kikuu hicho cha umma wa kushughulikia maandamano ya waungaji mkono wa Palestina.
Shirikisho la wafanyakazi la magari la Marekani (UAW) Local 4811, ambalo ni umoja wa wafanyakazi wa taaluma 48,000 katika kampasi kumi za mfumo wa chuo kikuu cha California na Maabara ya Kitaifa ya Lawrence Berkeley, zimetangaza Jumanne asubuhi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba UC Los Angeles "IKO KWENYE MGOMO rasmi."
Waandamanaji zaidi ya 50 wanaoshika bangola "UAW katika mgomo" walikuwa wakiandamana katikati ya Jengo la Dickson, limeripoti gazeti la wanafunzi wa chuo kikuu hicho, Daily Bruin siku ya Jumanne asubuhi, na kuongeza kuwa waandamanaji walikuwa wakitamka kwa sauti kaulimbiu za "L.A. ni mji wa umoja wa wafanyakazi" na "Chuo kikuu cha nani? Chuo kikuu chetu."
Baadhi ya waandamanaji waliokuwa wakiimba "Palestine Huru, huru" walikuwa wakizuia mlango wa jengo la kuegesha magari kwenye chuo hicho, kwa mujibu wa gazeti hilo.
UAW 4811 imesema kwenye tovuti yake kwamba "ilikuwa moja ya umoja wa wafanyakazi wa kwanza kabisa nchini Marekani kutoa wito wa kusimamishwa kwa mapigano na kupunguza vita huko Gaza" na wafanyakazi wa taaluma katika UC wanaunga mkono kwa nguvu haki ya waandaaji wa maandamano ya kupiga kambi katika haki yao ya kuandamana kwa amani.
Mamia ya wafanyakazi na wanataaluma wa chuo kikuu cha California wamekuwa wakimtaka Gene Block, mkuu wa UC Los Angeles, kujiuzulu kwa sababu ya mwitikio wa chuo kikuu hicho dhidi ya maandamano ya waungaji mkono wa Palestina kwenye chuo kikuu hicho.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma