IMF laongeza makadirio ya ukuaji wa pato la taifa la China mwaka 2024 hadi asilimia 5

(CRI Online) Mei 30, 2024

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeongeza makadirio ya ukuaji wa pato la taifa (GDP) la China mwaka 2024 kutoka makadirio ya awali ya ukuaji wa asilimia 4.6 iliyoyatoa Mwezi Aprili hadi asilimia 5.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF Bi. Gita Gopinath amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari baada ya timu ya shirika hilo kutembelea China kuanzia tarehe 16 hadi 28 mwezi huu.

Ameeleza kuwa marekebisho hayo ya makadirio yametokana na ukuaji wenye nguvu wa pato la taifa la China katika robo ya kwanza ya mwaka huu pamoja na sera mbalimbali zilizoanzishwa hivi karibuni.

Amesema China inafanya kazi muhimu na ya kiujenzi katika kusaidia urekebishaji wa madeni katika nchi zilizo hatarini na zenye pato la chini na kuhimiza kuhamia kuelekea uchumi wa kijani. IMF inatarajia kuendelea kushirikiana na China kwenye suala hili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha