

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akutana na Rais wa Tunisia Kais Saied
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Rais wa Tunisia Kais Saied kwenye Jumba la Wageni la Diaoyutai mjini Beijing, China, Mei 30, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Rais wa Tunisia Kais Saied ambaye yuko ziarani nchini China, kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 10 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu mjini Beijing siku ya Alhamisi ambapo amesema mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tunisia na kwamba katika miaka hiyo 60 iliyopita, uhusiano kati ya China na Tunisia umedumisha maendeleo thabiti na yenye manufaa kwa watu wa pande hizo mbili.
China inapenda kushirikiana na Tunisia ili kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuendeleza desturi ya urafiki na hali ya kuaminiana, kuendeleza mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kufanya kazi pamoja ili kuweka mazingira kwa ajili ya mustakbali bora zaidi wa siku za baadaye kwa nchi hizo mbili, Li amesema.
Ameongeza kuwa, China inaunga mkono kithabiti Tunisia katika kuchunguza kikamilifu njia ya maendeleo yenye umaalum wa Tunisia na inapinga kithabiti uingiliaji wa nje katika masuala ya ndani ya Tunisia.
Amesema China inapenda kushirikiana na Tunisia ili kuimarisha ushirikiano wenye matokeo halisi unaoongozwa na ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kupiga hatua thabiti katika miradi muhimu ya ushirikiano, na kupanua ushirikiano katika biashara na nishati mbadala.
China pia inapenda kushirikiana na Tunisia kufanya kila juhudi katika kujenga jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya na kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya ngazi ya juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja, Li amesema, huku akihimiza juhudi za pamoja kutoka pande hizo mbili ili kuimarisha uratibu na ushirikiano wa pande nyingi ili kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea.
Kwa upande wake Saied amesema tangu nchi hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepata maendeleo ya haraka, na ushirikiano umepata matokeo yenye matunda.
“Tunisia inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, inaiunga mkono China bila kuyumba yumba katika kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi yake, na inapinga vikali uingiliaji wa vikundi vya nje katika masuala ya ndani ya China,” Saied amesema.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Rais wa Tunisia Kais Saied kwenye Jumba la Wageni la Diaoyutai mjini Beijing, China, Mei 30, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma