Waziri wa Mambo ya Nje wa China atoa wito kwa China na Nchi za Kiarabu  kutilia maanani zaidi majukumu makuu manne

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Mohamed Salem Ould Merzouk, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mauritania, na Ahmed Aboul-Gheit, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, wakikutana na waandishi wa habari baada ya mkutano wa 10 wa mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu, mjini Beijing, China, Mei 30, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Mohamed Salem Ould Merzouk, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mauritania, wameongoza kwa pamoja mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu (CASCF) mjini Beijing siku ya Alhamisi ambapo mawaziri wa mambo ya nje na maofisa wa ujumbe wa nchi za Kiarabu waliohudhuria, wameshiriki katika mazungumzo ya kina juu ya kuharakisha ujenzi wa jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amebainisha kuwa tangu mkutano wa kwanza wa wakuu wa China na nchi za Kiarabu, maendeleo makubwa yamedhihirika katika ujenzi wa jumuiya ya China na nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja, na Uhusiano kati ya China na nchi za Kiarabu umeingia katika kipindi bora zaidi katika historia.

Ili kutekeleza kwa dhati makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa China na nchi za Kiarabu na matokeo ya mkutano huo, Wang amesema pande hizo mbili zinapaswa kuweka mkazo zaidi katika kutekeleza vizuri majukumu makuu manne: kuimarisha hali ya kuaminiana kimkakati na kuungana mkono kithabiti katika maslahi ya msingi ya kila mmoja wao; kuzidisha ushirikiano wenye manufaa halisi na kuhimiza hali ya kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja kwenye ngazi ya juu; kuimarisha uratibu wa kimataifa na kufanya juhudi kwa pamoja ili kudumisha mwelekeo sahihi wa usimamizi wa Dunia; na kuimarisha ujenzi wa jukwaa hilo na kuanzisha siku nzuri za baadaye kwa jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja.

Kwenye mkutano huo zilioneshwa kwa bendera za nchi za Kiarabu na ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zilizopelekwa kwenye kituo cha anga ya juu cha China, bendera hizo zikiwa kama zawadi zitazipa Nchi za Kiarabu baada ya mkutano huo kumalizika ili kuwa ukumbusho wa kudumu wa urafiki wa China na nchi za Kiarabu.

Mkutano huo umetoa Azimio la Beijing, mpango wa utekelezaji wa CASCF wa 2024-2026, na taarifa ya pamoja ya China na Nchi za Kiarabu kuhusu suala la Palestina. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mohamed Salem Ould Merzouk, Waziri wa Mambo ya Nje  naUshirikiano wa Mauritania, wakiongoza kwa pamoja mkutano wa 10 wa mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu, mjini Beijing, China, Mei 30, 2024. (Xinhua/Zhang Ling)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mohamed Salem Ould Merzouk, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mauritania, wakiongoza kwa pamoja mkutano wa 10 wa mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu, mjini Beijing, China, Mei 30, 2024. (Xinhua/Zhang Ling)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha