

Lugha Nyingine
Iran yasema hakuna njama wala vita vya kielektroniki iliyosababisha ajali ya helikopta iliyobeba rais Raisi
Watu wakiomboleza kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi kwenye madhabahu takatifu ya Imam Reza huko Mashhad, Kaskazini Mashariki mwa Iran, Mei 23, 2024. (Xinhua)
TEHRAN - Mkuu wa Majeshi wa Iran ametangaza Jumatano kwamba, hakuna njama wala vita vya kielektroniki iliyosababisha ajali ya helikopta iliyosababisha vifo vya Rais Ebrahim Raisi na watu wa msafara wake. Amesema, uchunguzi umethibitisha kwamba kwa mujibu wa vipimo vya ajali na mtawanyiko wa vipande vya helikopta hiyo, hakuna uwezekano wa kutokea kwa mlipuko uliosababishwa na njama wakati helikopta ikiwa angani au kabla ya kuanguka kwenye mlima.
Shirika la habari la Iran IRNA linasema, ripoti ya pili ya kamati kuu ya uchunguzi imeeleza kwa kina matokeo ya uchunguzi wake kuhusu ajali hiyo ya Mei 19 katika Jimbo la Azarbaijan Mashariki.
Ripoti hiyo pia imetupilia mbali uwezekano wa vita vya kielektroniki, ikieleza kutokuwepo kwa ushahidi. Hali ya hewa katika Mei 19 ilionekana kuwa nzuri kwa kanuni za Uoni wa Ndege wakati wa safari za ndege kutoka Tabriz hadi maeneo karibu na mpaka wa Azerbaijan, ingawa uchunguzi zaidi kuhusu hali ya ndege ya kurudi unaendelea.
Hakuna kasoro yoyote kuhusiana na ukarabati na matengenezo ya helikopta hiyo iliyobainika kuchangia ajali hiyo. Uzito wa helikopta, ikiwa ni pamoja na abiria na vifaa, ulikuwa ndani ya kikomo wakati wa kupaa na safarini. Mawasiliano yaliyorekodiwa kati ya marubani yalionyesha mawasiliano ya mwisho na helikopta iliyoanguka yalitokea sekunde 69 kabla ya tukio, na hakuna dharura iliyotangazwa.
Ripoti ya kwanza kutoka kwa kamati ya uchunguzi ilitolewa Mei 23. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian na Mohammad Ali Ale-Hashem, mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Iran katika Azarbaijan Mashariki, pia walikuwa ndani ya helikopta hiyo.
Rais Raisi alizikwa tarehe 23 Mei kwenye kaburi takatifu la Imam Reza huko Mashhad.
Watu wakiomboleza kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi kwenye madhabahu takatifu ya Imam Reza huko Mashhad, Kaskazini Mashariki mwa Iran, Mei 23, 2024. (Xinhua)
Watu wakiomboleza kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi huko Mashhad, Kaskazini Mashariki mwa Iran, Mei 23, 2024. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma