Miradi ya China yaleta utajiri katika Sahara

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 03, 2024

Mtaalamu wa China akiwaelekeza wafanyakazi wenyeji kupanda miche ya Juncao kwenye kituo cha kielelezo cha teknolojia ya ufugaji nchini Mauritania, Mei 27, 2024. (Xinhua)

Mtaalamu wa China akiwaelekeza wafanyakazi wenyeji kupanda miche ya Juncao kwenye kituo cha kielelezo cha teknolojia ya ufugaji nchini Mauritania, Mei 27, 2024. (Xinhua

YINCHUAN - Zhang Hong'en alifungasha sanduku la miche ya nyasi kutoka Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, Kaskazini Magharibi mwa China, kusafiri maelfu ya maili hadi nchi ya Mauritania, Afrika Magharibi na kuipanda kwenye udongo. Katika kipindi cha muda wa siku 50 tu, nyasi hizo za “maajabu” zilikua hadi kufikia urefu wa zaidi ya mtu mzima huku kila mche wa kukatwa ukiwa umegawanywa kwa wakulima kadhaa. Miezi mitatu baadaye, mimea hiyo ilifikia urefu wa mita 4, na kutoa lishe nyingi kwa mifugo ya wenyeji.

Ikiitwa "nyasi ya furaha" katika nchi nyingi, nyasi kubwa ya Juncao kutoka China ni zao la lishe kwa mifugo lenye mavuno mengi na inaweza kutoa lishe mbalimbali kwa mifugo.

"Kukuza nyasi nchini Mauritania hakika kutafaidisha wakulima na wafugaji," amesema Zhang, mkurugenzi wa kituo cha kielelezo cha teknolojia ya ufugaji nchini Mauritania.

Kwenye mkutano wa 10 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu uliofanyika Beijing siku ya Alhamisi, China imetangaza kuwa itajenga maabara 10 za pamoja na upande wa Nchi za Waarabu katika maeneo kama vile maisha na afya, AI, maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache, kilimo cha kisasa, safari ya anga ya juu na teknolojia ya habari.

Ikiwa ni sehemu ya juhudi za China za kuendeleza ushirikiano wa kilimo na nchi za Kiarabu, Wizara ya Biashara ya China na serikali ya Mkoa wa Ningxia zilianzisha kituo hicho cha kielelezo mwaka 2015 ili kutoa mwongozo wa kiufundi kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, uzalishaji malisho na usindikaji wa malisho nchini Mauritania.

Ukubwa wa eneo la upandaji wa Juncao katika kituo hicho umefikia hekta 0.2 na litapanuliwa hadi kufikia hekta 6.7 ifikapo mwisho wa mwaka huu.

"Kituo chetu cha kielelezo kitakuwa kituo cha kuzalisha miche ya Juncao, kutoa miche hiyo kwa Mauritania nchi nzima na kusaidia wakulima kupata lishe zaidi ya mifugo," amesema Zhang.

Ufugaji ni mojawapo ya nguzo kuu ya uchumi katika nchi ya Mauritania ambayo iko kwenye ukingo wa kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika.

Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, kituo hicho siyo tu kimegeuza hekta karibu 67 za ardhi katika kituo hicho cha kielelezo kuwa chemchemi lakini pia kimefanya maeneo mengi zaidi kuwa ya kijani nchini kote.

Kwa kuzingatia rasilimali za kipekee za baharini na mifugo na sera nzuri ya kutotoza ushuru ya Mauritania, Mao Guohua kutoka Mkoa huo wa Ningxia anapanga kujenga kiwanda cha kusindika nyama ya ngamia, nyama ya ng'ombe, kondoo na mazao ya baharini. Chakula kilichosindikwa tayari kitasafirishwa hadi China kwa ajili ya kuuzwa.

"Nilitembelea Mauritania mwezi Aprili na nina imani kubwa kuhusu mustakabali wa mradi huo," amesema Mao.

Zhang Hong'en, mkurugenzi wa kituo cha kielelezo cha teknolojia ya ufugaji nchini Mauritania, akikagua ukuaji wa Juncao kutoka China akiwa na mfanyakazi mwenyeji nchini Mauritania, Februari 19, 2024. (Xinhua)

Zhang Hong'en, mkurugenzi wa kituo cha kielelezo cha teknolojia ya ufugaji nchini Mauritania, akikagua ukuaji wa Juncao kutoka China akiwa na mfanyakazi mwenyeji nchini Mauritania, Februari 19, 2024. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha