

Lugha Nyingine
Sekta ya huduma za programu za kompyuta na TEHAMA ya China yashuhudia ukuaji wa mapato na faida
Mfanyakazi kutoka kampuni ya teknolojia akionyesha programu ya AI kwenye maonyesho ya Mkutano wa Uundaji wa Mambo ya Sayansi wa China (CSFC) 2023 mjini Beijing, China, Mei 30, 2023. (Xinhua/Chen Zhonghao)
BEIJING –Takwimu kutoka Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China zinaonyesha kuwa, sekta ya huduma za programu za kompyuta na teknolojia ya habari nchini China imepata ukuaji wa mapato na faida wa asilimia zaidi 10 mwaka hadi mwaka katika miezi minne ya kwanza ya Mwaka 2024.
Jumla ya faida ya sekta hiyo iliongezeka kwa asilimia 14.3 mwaka hadi mwaka na kufikia yuan bilioni 431.4 (kama dola za kimarekani bilioni 60.69) katika kipindi hicho, wakati mapato ya pamoja yaliongezeka kwa asilimia 11.6 hadi kufikia yuan trilioni 3.8, kwa mujibu wa wizara hiyo.
Jumla ya mapato ya sekta ndogo ya huduma ya teknolojia ya habari yaliongezeka kwa asilimia 13.2 mwaka hadi mwaka na kufikia yuan trilioni 2.5, ikichangia asilimia 65.9 ya mapato yote ya sekta hiyo.
Hasa, mapato ya pamoja ya teknolojia ya mawingu na data kubwa yaliongezeka kwa asilimia 14.3 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha Mwaka 2023, na kufikia yuan bilioni 410.7.
Takwimu hizo pia zimeonyesha kuwa mapato kutoka kwa bidhaa za programu za kompyuta na usalama wa habari yaliongezeka kwa asilimia 8.7 na asilimia 9.3 mtawalia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma