

Lugha Nyingine
Ofisa Mwandamizi wa Bunge la Umma la China atembelea Namibia
WINDHOEK - Cai Dafeng, naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, amefanya ziara nchini Namibia kuanzia Mei 30 hadi Juni 2 kutokana na mwaliko wa Bunge la Namibia. Katika ziara yake hiyo ya siku nne, Cai alifanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah, Spika wa Bunge Peter Hitjitevi Katjavivi, na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Namibia, Lukas Sinimbo Muha.
Cai amesema kuwa China na Namibia zimekuwa marafiki na washirika wazuri tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 34 iliyopita na kwamba pande hizo mbili zimedumisha urafiki wa dhati, kutendeana kwa usawa katika nyakati ngumu na nzuri, na kusonga mbele pamoja.
Amesema China itaendelea kuwa mshirika wa Namibia katika njia yake ya maendeleo na ustawishaji wa taifa, ili kuendeleza zaidi ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Namibia na kupata matokeo mapya.
Cai amewaeleza maofisa wa Namibia kuhusu hamasa ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, mkutano ujao wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), utakaofanyika Beijing majira yajayo ya Mpukutiko, pamoja na msukumo wa China wa ustawishaji wa taifa kupitia sayansi na elimu.
Upande wa Namibia umeishukuru China kwa uungaji mkono wake wa kujitolea wakati wa harakati zake za kupigania uhuru na ujenzi wa taifa, ukirejelea ahadi ya kufuata kwake kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kusisitiza jukumu muhimu la kufanya kazi pamoja kupitia Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na majukwaa kama vile FOCAC.
Maofisa hao wa Namibia pia wameeleza matumaini ya kujifunza kutoka kwa uzoefu wa maendeleo ya China na teknolojia zake za hali ya juu zilizoendelea, na kuimarisha zaidi ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.
Wakati wa kuwepo kwake huko Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Cai pia alitembelea Makumbusho ya Kumbukumbu ya Uhuru, ambayo yanaonesha mapambano ya nchi hiyo dhidi ya ukoloni na harakati zake za ukombozi wa nchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma