Wanasayansi wa kigeni waishukuru China kwa kuchangia fursa ya kuchunguza mwezi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2024

Picha hii iliyopigwa kutoka  video katika Kituo cha Udhibiti wa Anga ya Juu cha Beijing, China (BACC) Juni 2, 2024 ikionyesha mchanganyiko wa kifaa cha kutua na chombo cha kupanda cha chombo cha Chang'e-6 kikitua upande wa mbali wa mwezi. (Xinhua/Jin Liwang)

Picha hii iliyopigwa kutoka video katika Kituo cha Udhibiti wa Anga ya Juu cha Beijing, China (BACC) Juni 2, 2024 ikionyesha mchanganyiko wa kifaa cha kutua na chombo cha kupanda cha chombo cha Chang'e-6 kikitua upande wa mbali wa mwezi. (Xinhua/Jin Liwang)

BEIJING - Baada ya mchanganyiko wa kifaa cha kutua na kifaa cha kupanda cha chombo cha kuchunguza mwezi cha Chang'e-6 cha China chini ya msaada wa satelaiti ya kupokezana ya Queqiao-2, kufanikiwa kutua katika eneo lililopangwa kwenye Ncha ya Kusini-Aitken (SPA) ya mwezi siku ya Jumapili Asubuhi saa 12:23 asubuhi (Saa za Beijing) na kukusanya sampuli, wanasayansi wa kigeni walioshiriki katika kazi hiyo wameeleza shukrani zao kwa China kutokana na kupeleka vyombo vyao vya kisayansi mwezini.

Jukumu hilo la chombo cha Chang'e-6 limebeba mizigo minne kwenda mwezini iliyoundwa na kuandaliwa kupitia ushirikiano wa kimataifa, ukitoa fursa zaidi kwa wanasayansi wa kimataifa na kukusanyika ujuzi wa binadamu katika uchunguzi wa anga ya juu.

Vyombo vya kisayansi kutoka Ufaransa, Italia na Shirika la Anga ya Juu la Ulaya (ESA)/Sweden viko ndani ya chombo hicho kutua cha Chang'e-6.

"Asante China sana kwa kutupeleka mwezini," Sylvestre Maurice, mwanaanga Mfaransa kutoka Chuo Kikuu cha Toulouse, amesema baada ya kutazama mchakato wa kutua mwezini kwenye chumba cha udhibiti katika Kituo cha Kitaifa cha Uchunguzi wa Anga ya Juu cha Akademia ya Sayansi cha China siku ya Jumapili.

"Kutua kwa leo kunashangaza kabisa. Ni ngumu kutua kwenye sayari, na ni ngumu sana haswa mwezini. Usidhani ni rahisi. Kumbuka ni upande wa mbali wa mwezi ambapo hatuwezi kuona. Na China imebidi hata kuweka satelaiti nyingine ya kupokezana kutazama mchakato wa kutua. Vimetua pale vilipotaka, kwa hivyo ni mafanikio, kitu ambacho tumekuwa tukitafuta kwa miaka mingi," Maurice amesema.

"Upande wa mbali wa mwezi ni wa kipekee sana. Bonde la Ncha ya Kusini-Aitken ni bonde kubwa. Kulikuwa na mgongano mkubwa muda mrefu uliopita na kusababisha sehemu kubwa ya gamba kuondoka, kwa hivyo tunaweza kuwa tumetua karibu iwezekanavyo na gamba la mwezi," Maurice amesema.

Mathieu Grialou, mwakilishi kutoka shirika la anga ya juu la Ufaransa CNES, amesema chombo cha Chang'e-6 kitakuwa chombo cha kwanza cha kuleta sampuli kutoka upande wa mbali wa mwezi. "Tunafurahi sana kuwa sehemu ndogo ya jukumu hilo kubwa."

"Tunafuraha sana kushirikiana na China katika kazi hii kwani China sasa ni mshiriki muhimu kwenye anga ya juu," Grialou amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha