Waziri Mkuu wa Misri apewa jukumu la kuunda serikali mpya baada ya kujiuzulu kwa baraza la mawaziri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2024

Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa Januari 14, 2024 ikionyesha Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi jengo la ofisi ya mradi wa Eneo la Kiini cha Biashara (CBD) katika mji mkuu mpya wa utawala, Mashariki mwa Cairo, Misri. (Picha na Li Binghong/Xinhua)

Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa Januari 14, 2024 ikionyesha Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi jengo la ofisi ya mradi wa Eneo la Kiini cha Biashara (CBD) katika mji mkuu mpya wa utawala, Mashariki mwa Cairo, Misri. (Picha na Li Binghong/Xinhua)

CAIRO - Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi amemuagiza Waziri Mkuu Mostafa Madbouly kuunda serikali mpya baada ya waziri mkuu huyo kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa baraza lake la mawaziri siku ya Jumatatu, ofisi ya rais wa Misri imetangaza katika taarifa yake.

Madbouly amepewa jukumu la kuanzisha serikali mpya inayoundwa na watu wenye sifa nzuri ya juu, wenye uwezo, na wenye uzoefu, ili kufikia malengo mengi, imesema taarifa hiyo.

Rais Sisi ameamuru kwamba serikali mpya inapaswa kuweka kipaumbele cha juu katika kudumisha usalama wa nchi ya Misri kwa kuzingatia changamoto zilizopo za kikanda na kimataifa, kuendeleza sekta za afya na elimu, kuendelea na juhudi za kuwahamasisha watu kushiriki kwenye mambo ya kisiasa, na kupata mafanikio zaidi kwenye msingi wa awali katika usalama, utulivu na mapambano dhidi ya ugaidi.

Pia ameliagiza baraza jipya la mawaziri kuendelea kufanya mageuzi ya kiuchumi, kuweka mkazo katika kuvutia na kuongeza uwekezaji, kuhamasisha ukuaji wa sekta binafsi, na kuzuia kupanda kwa bei na mfumuko wa bei.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa serikali ya sasa bado itaendelea kufanya kazi hadi itakapoundwa kwa serikali mpya.

Tovuti ya habari ya kiserikali ya Ahram Online imetoa habari zikisema kuwa, haya ni mabadiliko ya nne ya baraza la mawaziri yakiongozwa na Madbouly, ambaye amekuwa waziri mkuu tangu Mwaka 2018. Mabadiliko ya mwisho ya baraza la mawaziri yalikuwa Agosti 2022.

Rais Sisi alianza kushika madaraka yake ya rais wa awamu ya tatu mfululizo mwezi Aprili, na muda wake huo utaendelea hadi Mwaka 2030. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha