Msimamo wa China kuhusu mgogoro wa Ukraine ni kuhimiza mazungumzo ya amani: Waziri wa Mambo ya Nje wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2024

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi siku ya Jumanne mjini Beijing alipokutana na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amefafanua msimamo thabiti wa China kuhusu mgogoro wa Ukraine, akisisitiza kuwa China inatilia maanani kuhimiza mazungumzo ya amani, na ingawa mazingira ya mazungumzo ya amani bado hayajapatikana, China haitaacha kamwe juhudi zake kwa ajili ya amani.

China pia inahimiza na kuunga mkono jitihada na juhudi zote duniani ambazo zinasaidia kupunguza hali ya wasiwasi ya kikanda na kutimiza amani, ameongeza Wang.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema kuwa China inatilia maanani kazi ya Uswisi kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Kilele wa Amani nchini Ukraine, na mara nyingi imetoa mapendekezo ya kiujenzi kwa upande wa Uswisi, ambayo upande wa Uswisi daima umetoa maoni chanya na shukrani.

"Kuna mikutano mingi ya kilele duniani leo. Kama kushiriki na namna ya kushiriki, China itajiamuliwa kwa kulingana na msimamo wake," Wang ameongeza.

Mei 23, Wang Yi alikutana na Celso Amorim, mshauri maalum wa Rais wa Brazil, mjini Beijing. Pande hizo mbili zilibadilishana maoni kwa kina juu ya kusukuma suluhu ya kisiasa ya mgogoro wa Ukraine na kutoa wito wa kupunguza kuchochea hali ya mgogoro huo, na kufikia waraka wa maelewano sita ya pamoja.

China inaamini kwamba Dunia sasa inahitaji kutoa sauti zisizo na upendeleo kwa upande wowote, zenye uwiano, chanya na za kiujenzi zaidi juu ya mgogoro wa Ukraine, Wang amebainisha, huku akiongeza kuwa kwa ajili hiyo, hivi karibuni China na Brazil zilitoa kwa pamoja waraka wa "Maelewano ya Pamoja kati ya China na Brazil juu ya Suluhu ya Kisiasa kwa Mgogoro wa Ukraine."

Katika wiki moja tu, nchi 45 kutoka mabara matano zimeitikia vyema "maelewano hayo sita ya pamoja" kwa njia tofauti, kati ya hizo nchi 26 zimethibitisha kujiunga nayo au zinachunguza kwa makini namna ya kujiunga. “Russia na Ukraine pia zimethibitisha mengi yaliyomo katika maelewano haya sita ya pamoja,” Wang ameongeza.

Amesema, hii kwa mara nyingine inaonyesha kwamba maelewano haya sita ya pamoja yanakidhi matarajio ya pamoja ya nchi nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha