Slovenia yaitambua rasmi Palestina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2024

Spika wa Bunge la Slovenia, Urska Klakocar Zupancic (Kulia, Nyuma) akihudhuria kikao cha bunge mahsusi kwa ajili ya kuitambua Palestina mjini Ljubljana, Slovenia, tarehe 4 Juni 2024. (Bozidar Kolar/STA/ Xinhua)

LJUBLJANA - Bunge la Slovenia limepiga kura siku ya Jumanne kuidhinisha pendekezo la kuitambua rasmi Palestina, hatua ambayo chombo hicho cha bunge kimesema, inatarajiwa kusaidia kukomesha ghasia huko Gaza.

Wabunge 52 kati ya wote 90 wamepiga kura hiyo ya kuitambua Palestina na kuifanya Slovenia ambayo kwa sasa ni nchi mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kuwa nchi ya nne ya Ulaya baada ya Hispania, Norway na Ireland kufanya uamuzi huo.

"Jamhuri ya Slovenia imeitambua Palestina kuwa taifa huru," Spika wa Bunge Urska Klakocar Zupancic amesema baada ya kupigwa kwa kura hiyo.

"Kutambuliwa kwa Palestina kunaongeza sifa ya Slovenia ya kuwa taifa linaloheshimu sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa na wakati huo huo kutoa shinikizo kwa pande zote mbili: kwa Israel kuacha mashambulizi huko Gaza na kwa Hamas kuwaachilia mateka." Waziri wa Mambo ya Nje wa Slovakia Tanja Fajon ameliambia Bunge hilo kabla ya zoezi la kupiga kura.

"Tunafanya kazi kuelekea amani na suluhu ya mataifa mawili," ameongeza.

Wabunge wengi wa chama kikuu cha upinzani, Slovenian Democratic Party (SDS) chenye mrengo wa kati-kulia, hawakuhudhuria kikao hicho cha bunge lakini walipendekeza kura ya maoni kuahirisha kura hiyo ya bunge kwa angalau siku 30. Pendekezo lao lilikataliwa mapema siku hiyo ya Jumanne na wabunge walio wengi bungeni.

Norway, Ireland na Hispania zilitoa tangazo lililoratibiwa Mei 22, na kutangaza kuitambua rasmi Palestina kuanzia Mei 28. Lakini uamuzi huo ulilaaniwa na Israel.

Hadi sasa, nchi zaidi ya 140 tayari zimelitambua taifa la Palestina, ikiwakilisha zaidi ya theluthi mbili ya nchi wanachama wote wa Umoja wa Mataifa. 

Waziri Mkuu wa Slovenia, Robert Golob (Mbele) akihudhuria kikao cha bunge mahsusi kwa ajili ya kuitambua Palestina mjini Ljubljana, Slovenia, tarehe 4 Juni 2024. (Bozidar Kolar/STA/ Xinhua)

Waziri Mkuu wa Slovenia, Robert Golob (Mbele) akihudhuria kikao cha bunge mahsusi kwa ajili ya kuitambua Palestina mjini Ljubljana, Slovenia, tarehe 4 Juni 2024. (Bozidar Kolar/STA/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha