Ubalozi wa China watoa mahitaji kwa watoto wa Zimbabwe

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2024

Watoto wakishiriki kwenye hafla ya makabidhiano ya zawadi za msaada  kwa Mfuko wa Dzikwa Trust Fund mjini Harare, Zimbabwe, tarehe 3 Juni 2024. Xinhua/Tafara Mugwara)

Watoto wakishiriki kwenye hafla ya makabidhiano ya zawadi za msaada kwa Mfuko wa Dzikwa Trust Fund mjini Harare, Zimbabwe, tarehe 3 Juni 2024. Xinhua/Tafara Mugwara)

HARARE - Ubalozi wa China nchini Zimbabwe umetoa zawadi za mahitaji kwa Mfuko wa Dzikwa Trust Fund, shirika la kutoa misaada ya kielimu la Zimbabwe, siku ya Jumatatu mjini Harare, Zimbabwe. Msaada huo ni pamoja na vyakula na vitu mbalimbali vya usafi. Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding amekabidhi rasmi vitu hivyo kwa mfuko huo wa Zimbabwe.

Mkurugenzi wa programu wa Mfuko wa Dzikwa Trust Fund, Oili Wuolle, ametoa shukrani zake kwa msaada huo, akisema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa watoto hao ambao wengi wao ni yatima wanaoishi na familia kubwa.

"Tunathamini sana mchango huu kwa sababu umetuletea chakula na vitu vya usafi kwa jiko letu kwa mwezi mmoja kamili," Wuolle ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua baada ya kupokea msaada huo.

Msaada huo pia ni pamoja na simu janja ili kusaidia mipango ya shule ya mafunzo ya ustadi wa kidijitali.

Wuolle amesema, uungaji mkono kutoka Ubalozi wa China umekuwa muhimu katika kusomesha watoto hao, na wanafunzi wanne wa shirika hilo kwa sasa wanasoma katika vyuo vikuu vya China.

"Katika utamaduni wa China, elimu ni muhimu sana, na kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Zimbabwe, ndiyo njia pekee ya kujitoa kutoka kwenye matatizo na ni njia pekee ya kujitegemea," amesema.

Katika hotuba yake, Balozi Zhou amesema kuwa Ubalozi wa China umeanzisha shughuli mfululizo za hisani katika kuwasaidia vijana wa Zimbabwe kutafuta mustakabali mzuri.

"Ninaamini kwamba kupitia juhudi zetu za pamoja, Zimbabwe itafikia lengo lake la kufikia hadhi ya uchumi wa mapato ya kati hivi karibuni, na watu wetu wa pande zote mbili wataungana katika kujenga jumuiya ya pamoja yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu," Zhou amesema.

Watoto  wakicheza ngoma kwenye hafla ya makabidhiano ya zawadi za msaada kwa   Mfuko wa Dzikwa Trust Fund mjini Harare, Zimbabwe, tarehe 3 Juni 2024. Xinhua/Tafara Mugwara)

Watoto wakicheza ngoma kwenye hafla ya makabidhiano ya zawadi za msaada kwa Mfuko wa Dzikwa Trust Fund mjini Harare, Zimbabwe, tarehe 3 Juni 2024. Xinhua/Tafara Mugwara)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha