

Lugha Nyingine
Uzoefu na kampuni za China waboresha ustadi wa vijana wa Cameroon
Mfanyakazi wa Cameroon akifanya kazi kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa awamu ya II wa Bandari ya Kina Kirefu ya Kribi, Cameroon, Aprili 22, 2024. (Picha na Kepseu/Xinhua)
YAOUNDE - Jua likiwa linaangaza vyema katika mji wa Kribi, Kusini mwa Cameroon. Wachina na Wacameroon walikuwa wakifanya kazi bega kwa bega kwa masikilizano katika eneo kubwa la ujenzi kwenye Bandari ya Kina kirefu ya Kribi, ambapo Kampuni ya Uhandisi wa Bandari ya China (CHEC) inajenga awamu ya II ya mradi wa bandari hiyo.
Kwa kawaida, kampuni ya CHEC inawapanga kufanya kazi pamoja wafanyakazi wa Cameroon na wenzao Wachina wenye uzoefu mkubwa, ambao wanawasaidia kufanya kazi zao mpaka wanapokuwa na uwezo wa kufanya kazi hizo bila ya msaada.
Eric Defo Fotso na Larissa Ekale Koule, wafanyakazi wa Cameroon katika CHEC, wameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba mazingira kama hayo ya kazi yamechangia kwa kiasi kikubwa uhamishaji wa ujuzi na maendeleo ya ujuzi wa wafanyakazi wenyeji.
"Nimejifunza mengi linapokuja suala la majukumu ya usimamizi na jinsi ya kusimamia shughuli kwenye eneo la ujenzi. Ni fahari kubwa kwangu kufanya kazi katika mradi kama huu kwa nchi yangu na pia kwa CHEC," amesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 28. Koule, ambaye kazi yake kubwa ni kuhakikisha wafanyakazi wote kwenye eneo la ujenzi wanakuwa na afya njema na hakuna anayeugua majeraha yanayohusiana na kazi.
Fotso, mwenye umri wa miaka 34, anaratibu miradi kwenye eneo la ujenzi.
"Jambo la kwanza nililojifunza ni jinsi ya kufanya kazi katika mazingira ya tamaduni nyingi. Kwa kuzingatia kwamba mradi unafuata viwango vya China, kwanza tunatakiwa kuwa na uelewa na matumizi kulingana na viwango vya China," amesema.
Jonas Hadomaha mwenye umri wa miaka 31, sasa anafanya kazi katika geti la kisasa la tozo za ushuru wa barabara kuu ya Kribi-Lolabe, ambayo pia ni sehemu ya mradi huo. Alianza kufanya kazi CHEC akiwa ni mkarimani lakini akapata ujuzi na maarifa kutokana na ushirikiano na wenzake wa China.
"Hii ni mara yangu ya kwanza kufanya kazi na kampuni inayosimamia barabara kuu, na nimejifunza mengi kuhusu utendakazi wa barabara kuu," amesema.
Kama ilivyo kwa Hadomaha, Fotso na Koule, maelfu ya watu wa Cameroon wameajiriwa na kampuni za China, ambazo huwafundisha kazini au kupitia programu rasmi.
Mbali na kutoa fursa za ajira kwa wenyeji, kampuni za China zinasaidia vijana wa Cameroon kuboresha ustadi wao na kuchangia vyema katika maendeleo ya viwanda ya nchini humo.
Mafundi wa Cameroon na China wakizungumza kwenye chumba cha mashine kwenye kiwanda cha kusafisha maji ya kunywa huko Bafoussam, Cameroon, Februari 20, 2024. (Picha na Kepseu/Xinhua)
Mafundi wa Cameroon na China wakizungumza kwenye chumba cha mashine kwenye kiwanda cha kusafisha maji ya kunywa huko Bafoussam, Cameroon, Februari 20, 2024. (Picha na Kepseu/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma