Mazingira ya ikolojia, sifa ya hewa na ya maji yaboreshwa nchini China Mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 06, 2024

Picha iliyopigwa tarehe 5 Juni 2024 ikionyesha wanakijiji wakivuna maua ya ottelia acuminata kwenye kituo cha upandaji maua ya ottelia acuminata katika Wilaya ya Eryuan ya Eneo linalojiendesha la Kabila la Wabai la Dali, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China. (Picha na Luo Xincai/Xinhua)

Picha iliyopigwa tarehe 5 Juni 2024 ikionyesha wanakijiji wakivuna maua ya ottelia acuminata kwenye kituo cha upandaji maua ya ottelia acuminata katika Wilaya ya Eryuan ya Eneo linalojiendesha la Kabila la Wabai la Dali, Mkoa wa Yunnan, Kusini-Magharibi mwa China. (Picha na Luo Xincai/Xinhua)

BEIJING - China imeripoti ufanisi bora zaidi wa ulinzi wa mazingira Mwaka 2023, huku kukiwa na kuendelea kuboreshwa kwa sifa ya hewa na sifa ya maji. Katika miji 339 inayofuatiliwa na Wizara ya Ikolojia na Mazingira ya China, PM2.5, ambacho ni kiashiria muhimu cha uchafuzi wa hewa, kilikuwa mikrogramu 30 kwa kila mita za ujazo Mwaka 2023, ikiwa ni karibu mikrogramu 3 kwa kila mita ya ujazo ambayo ni chini kutoka kwenye lengo la mwaka.

Taarifa ya ikolojia na mazingira iliyotolewa Jumatano na Wizara hiyo imesema, takwimu hizo zimeshuka kwa asilimia 28.6 tokea Mwaka 2016, ikionyesha mwelekeo wa kuendelea kuboreshwa kwa sifa ya hewa.

Kwa upande wa maji ya juu ya ardhi, asilimia 89.4 ya sehemu zinazofuatiliwa zilikuwa na sifa nzuri, ambayo ni juu ya ngazi ya tatu katika mfumo wa sifa ya maji ya ngazi tano wa China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.5 mwaka hadi mwaka.

Taarifa hiyo pia imeonesha kuwa maeneo ya maji ya bahari chini ya mamlaka ya China yenye sifa nzuri ya juu yalifikia asilimia 97.9, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.5.

Jana siku ya Jumatano ilikuwa Siku ya Mazingira ya Dunia, ambayo ni siku ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuhimiza watu wote duniani waongeze uelewa na hatua za kulinda mazingira ya sayari ya Dunia.

Siku hiyo ya Mazingira ya Dunia kwa mwaka huu imesisitiza zaidi ufufukaji wa ardhi, kupunguza hali ya jangwa kwenye ardhi na kuongeza uwezo wa kukabiliana na hali ya ukame.

China imerejesha hali ya ikolojia kwenye maeneo ya ardhi za hekta milioni 6.7 ikiwa ni pamoja na milima, mito, misitu, mashamba, maziwa, mbuga na majangwa, amesema ofisa wa Wizara ya Maliasili ya China kwenye shughuli ya mada mahsusi iliyoandaliwa na ofisi ya ujumbe wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa nchini China siku ya Jumatatu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha