Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Venezuela

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 06, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Yvan Gil Pinto mjini Beijing, China, Juni 5, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING- Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Yvan Gil Pinto mjini Beijing siku ya Jumatano, ambapo amesema kuwa chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wa nchi zote mbili, uhusiano wa China na Venezuela umekuwa ukiendelea kwa mwelekeo dhahiri zaidi na maudhui ya mambo zaidi na msukumo mkubwa zaidi.

Huku akibainisha kuwa mwaka huu ni mwaka wa 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Venezuela, Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema pande zote mbili zinapaswa kushikilia makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili kama mwongozo, kufanya majumuisho ya uzoefu wa mafanikio ya miaka 50 iliyopita ya uhusiano wa pande mbili, kufanya mipango ya kimkakati kwa mtazamo wa siku za baadaye, na kuingiza mambo mapya katika uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati wa siku zote kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Yvan Gil Pinto amesema kuwa Venezuela daima inashikilia kwa uthabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inaishukuru kwa dhati China kwa uungaji mkono wake muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kimaisha ya Venezuela.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Yvan Gil Pinto mjini Beijing, China, Juni 5, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Yvan Gil Pinto mjini Beijing, China, Juni 5, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha