“Kijiji cha Kwanza cha China cha Kuponi ya Kaboni” inayoweza kuuzwa na kupata pesa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 06, 2024

Mfano wa  kuponi ya kaboni ya misitu ya Sanming. Picha na Ouyang Yijia/People’s Daily Online

Mfano wa kuponi ya kaboni ya misitu ya Sanming. Picha na Ouyang Yijia/People’s Daily Online

Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China mwaka 2022, katika Kijiji cha Changkou cha Wilaya ya Jiangle ya Mji wa Sanming wa Mkoa wa Fujian, China, kila mwanakijiji alipokea bahasha nyekundu maalumu yenye pesa za Yuan 150 ambazo ni gawio la faida kutokana na Yuan 140,000 (sawa na dola 19,322 hivi za Marekani) kilizopata kijiji chao kwa kupitia kuponi ya kaboni ya misitu Mwaka 2021.

Kuponi ya Kaboni ya Misitu ni uthibitisho wa haki ya kufaidika kutokana na kupunguza utoaji wa kaboni misituni, ambayo ni sawa na “kadi” ya umiliki wa mali na ya biashara kwa kila eneo la misitu lililopunguza utoaji wa kaboni misituni. Tarehe 18 Mei, 2021, kijiji cha Changkou kilipokea Kuponi ya kaboni ya namba “0000001”, ambayo inamaanisha kijiji hiki kimekuwa “kijiji cha kwanza cha China cha Kuponi ya kaboni ya misitu”.

Wanakijiji wa Kijiji cha Changkou wakiwa wamepokea gawio  la kwanza la  la faida za kuponi ya kwanza ya kaboni ya misitu. (Picha imetolewa na mhojiwa)

Wanakijiji wa Kijiji cha Changkou wakiwa wamepokea gawio la kwanza la la faida za kuponi ya kwanza ya kaboni ya misitu. (Picha imetolewa na mhojiwa)

Mnamo 1997, Xi Jinping, wakati huo akiwa naibu katibu mkuu wa kamati ya Chama ya Mkoa wa Fujian alipofanya ziara huko Sanming alisisitiza kuwa, ni lazima tuwe na uelewa kwamba “kulinda ikolojia ya mazingira ya asili ni kulinda nguvu za uzalishaji, kuboresha mazingira ya asili ni kuendeleza nguvu za uzalishaji”. Tarehe 11, Aprili, 1997, Xi alipofanya ziara kwenye Kijiji cha Changkou aliwaambia viongozi wa kijiji hicho kuwa, “Milima ya kijani na mito safi ni hazina yenye thamani isiyohesabika.”

Xi pia alitoa agizo kuwa, misitu ya kiikolojia, pia ni shughuli za siku za baadaye. Ni lazima tufanye vizuri kazi za sekta ya misitu na ikolojia ya misitu, na kuweka uhifadhi wa udongo na maji kwenye nafasi muhimu, vinginevyo kutakuwa na hali ya kutelekezwa kwa milima mingi, ambapo hatutapata chochote siku za baadaye.

Jiwe la kumbukumbu la Kijiji cha Changkou likiwa limeandikwa  agizo la Xi Jinping. (Picha na Lin Wenbin), Chanzo: Sanming Daily

Jiwe la kumbukumbu la Kijiji cha Changkou likiwa limeandikwa agizo la Xi Jinping. (Picha na Lin Wenbin), Chanzo: Sanming Daily

Mpaka hivi leo, wanakijiji wa Kijiji cha Changkou bado wanakumbuka agizo la Xi. Wamedhamiria kuendelea kutafuta njia mpya zaidi za kupunguza utoaji wa kaboni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha