Uwanja wa ndege unaojengwa kwa msaada wa China mjini Gwadar, Pakistan waanza majaribio ya safari za ndege

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 06, 2024

Picha hii ikionyesha ndege baada ya kumaliza majaribio ya safari yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gwadar unaojengwa kwa msaada wa China katika mji wa bandari wa kusini magharibi wa Gwadar, Pakistan, Juni 4, 2024. (Timu ya Usimamizi wa Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gwadar unaojengwa kwa msaada wa China/Xinhua)

ISLAMABAD - Uwanja wa Ndege Mpya wa Kimataifa wa Gwadar unaojengwa kwa msaada wa China nchini Pakistan umeanza kufanya majaribio ya safari za ndege ya siku tano kuanzia siku ya Jumanne, ikiashiria kuwa mradi huo unakaribia kuingia katika hatua ya mwisho ya kukamilika, timu ya usimamizi wa mradi huo wa uwanja imesema.

Ding Kan, mkuu wa timu hiyo, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba kazi ya majaribio ya safari za ndege za uwanja huo, unaojengwa chini ya Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC) na uko katika mji wa bandari wa kusini magharibi wa Gwadar, imeandaliwa na kutekelezwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Pakistan. (CAA).

Lengo kuu la shughuli hiyo ni kuangalia uwekaji viwango sawia na usalama wa vifaa vya urambazaji vya mradi, usaidizi wa urambazaji, taratibu za safari za ndege na ufanisi wa muundo wa barabara, amesema, huku akiongeza kuwa majaribio hayo ni hatua muhimu ya ujenzi wa mradi huo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa kwa usalama na ubora wa safari za ndege katika uwanja huo mpya wa ndege.

Kufuatia kukamilika kwa majaribio hayo ya safari za ndege, mradi huo utaingia katika hatua ya mwisho ya kukamilishwa, na inatarajiwa kuwa uwanja huo wa ndege utakamilika na kukabidhiwa kwa serikali ya Pakistan mwaka huu wa 2024, meneja huyo wa China amesema.

Ujenzi wa uwanja huu wa ndege wa kiwango cha 4F, ulianza Oktoba 2019, ni moja ya miradi mikuu ya CPEC.

Baada ya kukamilika, utakuwa alama ya ujenzi wa mambo ya kisasa huko Gwadar, ambayo inaweza kuboresha kwa kiasi kikubwa hali ya miundombinu huko Gwadar na utaweka msingi bora wa maendeleo ya baadaye ya bandari pamoja na mji huo. 

Ndege ikikaribishwa kwa heshima ya kumwagiliwa maji yanayounda lango la maji baada ya kumaliza majaribio ya safari yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gwadar unaojengwa kwa msaada wa China katika mji wa bandari wa kusini magharibi wa Gwadar, Pakistan, Juni 4, 2024. (Timu ya Usimamizi wa Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gwadar unaojengwa kwa msaada wa China/Xinhua)

Ndege ikiwa imeegeshwa baada ya kumaliza majaribio ya safari yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gwadar unaojengwa kwa msaada wa China katika mji wa bandari wa kusini magharibi wa Gwadar, Pakistan, Juni 4, 2024. (Timu ya Usimamizi wa Mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gwadar unaojengwa kwa msaada wa China/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha