Mashindano ya lugha ya Kichina yafanyika nchini Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 06, 2024

Mshiriki akishindana katika Shindano la Umahiri wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo wa Ethiopia mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 5 Juni 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Shindano la Umahiri wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo wa Ethiopia lililoandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Ethiopia, Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa (AAU) na Taasisi ya Confucius katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi cha FDRE (TVTI) limefanyika mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, siku ya Jumatano.

Kwenye fainali ya shindano hilo la Mwaka 2024 nchini Ethiopia, washiriki wamepewa changamoto ya kutoa hotuba, kujibu maswali mawili kuhusiana na utamaduni wa China, na kuwasilisha maonyesho ya vipaji mbele ya maofisa waandamizi wa serikali ya Ethiopia, jumuiya ya wanadiplomasia wa China nchini humo pamoja na wasomi na wanafunzi wenzao wa lugha ya Kichina kutoka katika Taasisi za Confucius nchini humo.

Wanafunzi jumla ya 11 wa Ethiopia kutoka kote nchini wameshiriki kwenye shindano hilo la kila mwaka la kuongea Lugha ya Kichina na kufanya maonyesho ya Utamaduni wa China katika TVTI.

Alemu Seyoum, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa lugha ya Kichina kutoka Taasisi ya Confucius katika AAU, amepata tuzo ya mshindi wa kwanza huku akipigiwa makofi ya shangwe kutoka kwa watazamaji kutokana na hotuba yake yenye nguvu na onyesho mahiri la muziki wa jadi wa China.

Akihutubia hafla ya kutunuku washindi wa shindano hilo la mwaka huu, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Elimu wa Ethiopia Kora Tushune amesisitiza mchango mkubwa wa mawasiliano ya lugha na ya kitamaduni katika kukuza uhusiano kati ya watu wa China na Ethiopia.

"Kuanzishwa kwa Taasisi ya Confucius katika AAU na kufunguliwa kwa vituo kama hivyo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini kumeunda madaraja ya kijamii na kitamaduni, na kumekuza diplomasia ya umma, uelewa wa duniani na uhusiano kati ya watu," Tushune amesema.

Shen Qinmin, Kaimu Balozi wa China nchini Ethiopia, kwa upande wake ametoa wito hasa kwa washiriki na wanafunzi wengine wa lugha ya Kichina kutumika kama madaraja unganishi kati ya watu ndugu wa pande hizo mbili.

Washiriki wakionesha vyeti vyao baada ya Shindano la Umahiri wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo wa Ethiopia mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 5 Juni 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Elimu wa Ethiopia Kora Tushune (Kushoto) akizungumza kwenye Shindano la Umahiri wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo wa Ethiopia mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 5 Juni 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Elimu wa Ethiopia Kora Tushune (Kushoto) akizungumza kwenye Shindano la Umahiri wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo wa Ethiopia mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 5 Juni 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Mshiriki akishindana katika Shindano la Umahiri wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo wa Ethiopia mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 5 Juni 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Mshiriki akishindana katika Shindano la Umahiri wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo wa Ethiopia mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 5 Juni 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

Mshiriki akitumbuiza kwenye Shindano la Umahiri wa Lugha ya Kichina la "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo wa Ethiopia mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 5 Juni 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha