Wakuu wa nchi za China, Kyrgyzstan na Uzbekistan wapongeza kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali kuhusu mradi wa reli

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 07, 2024

Rais wa China Xi Jinping akipongeza kwa njia ya video kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali mjini Beijing, China kuhusu mradi wa reli ya China-Kyrgyzstan-Uzbekistan, Juni 6, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov na Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev siku ya Alhamisi wamepongeza kwa njia ya video kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali kuhusu mradi wa reli ya China-Kyrgyzstan-Uzbekistan.

Rais Xi amesema reli hiyo ni mradi wa kimkakati wa mafungamano ya mawasiliano kati ya China na Asia ya Kati na mradi wa kihistoria wa juhudi za ushirikiano wa nchi hizo tatu chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Amesema kusainiwa kwa makubaliano hayo kati ya serikali tatu kutatoa msingi imara wa kisheria kwa ujenzi wa mradi huo, ikionesha mradi wa reli hiyo kubadilika kuwa hali halisi kutoka matarajio, na kuionesha Dunia dhamira thabiti ya nchi hizo tatu kuendeleza ushirikiano na kutafuta maendeleo kwa pamoja.

“China ingependa kujiunga na Kyrgyzstan na Uzbekistan katika kufanya maandalizi mbalimbali ya kuanzisha ujenzi wa mradi huo na kukamilisha mapema njia hiyo ya reli ya kimkakati inayoweza kuleta manufaa kwa nchi hizo tatu na watu wake na kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya eneo hilo” Rais Xi amesema.

Kwa upande wake Japarov amesema reli hiyo ni mradi kinara wa nchi hizo tatu katika ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, mara utakapokamilika, itakuwa njia mpya ya usafiri inayounganisha Asia na Ulaya na nchi za Ghuba ya Uajemi, ambayo ina umuhimu mkubwa katika kuhimiza mafungamano ya mawasiliano na kuimarisha mawasiliano katika sekta za uchumi na biashara kati ya nchi zilizoko kwenye kando za njia hiyo ya reli hata katika kanda zima.

Naye Mirziyoyev amesema hafla hiyo ya kutiwa saini ni yenye umuhimu wa kihistoria, na ni hatua kubwa iliyopigwa kwa kufuata hali halisi kwa kuelekea ujenzi wa mafungamano ya mawasiliano ya kikanda.

Amesema reli hiyo itakuwa njia fupi zaidi ya kwenye nchi kavu kati ya China na nchi za Asia ya Kati, na pia itafungua masoko makubwa ya nchi za Asia Kusini na Mashariki ya Kati.

Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov akipongeza kwa njia ya video kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali mjini Beijing, China kuhusu mradi wa reli ya China-Kyrgyzstan-Uzbekistan, Juni 6, 2024. (Xinhua/Xing Guangli)

Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev akipongeza kwa njia ya video kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali mjini Beijing, China kuhusu mradi wa reli ya China-Kyrgyzstan-Uzbekistan, Juni 6, 2024. (Xinhua/Xing Guangli)

Hafla ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali kuhusu mradi wa reli ya China-Kyrgyzstan-Uzbekistan ikifanyika mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Xing Guangli)

Hafla ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya serikali kuhusu mradi wa reli ya China-Kyrgyzstan-Uzbekistan ikifanyika mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Xing Guangli)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha