Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Rais wa Cuba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 07, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Cuba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bruno Rodriguez Parrilla, mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Cuba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bruno Rodriguez Parrilla, siku ya Alhamisi mjini Beijing ambapo amesema kuwa China na Cuba ni marafiki wazuri wanaoaminiana, makomredi wazuri wanaochangia maono sawa, na ndugu wema ambao wanachangia shida na raha.

Ameongeza kuwa pande hizo mbili zilifikia makubaliano muhimu juu ya kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Cuba yenye mustakabali wa pamoja.

China inapongeza sana Cuba kushikilia ukweli na kupinga umwamba, na kwamba Cuba daima inasimama kidete kwa msimamo halali wa China katika masuala ya kimataifa ya pande nyingi. China inaiunga mkono kithabiti Cuba kutetea mamlaka yake na kupinga uingiliaji kati wa nchi za kigeni, na itaendelea kupinga vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba, Wang ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema.

Amesema, China inapenda kushirikiana na Cuba kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuendeleza uhusiano maalum wa kirafiki kati ya vyama na nchi hizo mbili, na kutoa mchango kwa ajili ya kuhimiza mambo ya ujamaa duniani na kulinda amani ya Dunia.

Kwa upande wake Rodriguez amesema uhusiano maalum wa kirafiki kati ya Cuba na China unapata uungaji mkono mkubwa wa umma kwa ajili ya urafiki mzuri kati ya watu wa pande hizo mbili.

Amesema Cuba inaishukuru kwa dhati China kwa uungaji mkono wake mkubwa katika kupinga vikwazo na uingiliaji wa Marekani na kukabiliana na matatizo ya muda katika uendeshaji wa uchumi, na itaendelea kushikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja.

Amesema Cuba inapenda kushirikiana na China kujenga jumuiya ya Cuba na China yenye mustakabali wa pamoja, kutoa kipaumbele cha juu katika kujenga kwa pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kulinda mamlaka na uhuru wa nchi zinazoendelea pamoja na mambo ya ujamaa.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya China na nchi za Latin Amerika na masuala mengine zinayoyafuatilia kwa pamoja. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Cuba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bruno Rodriguez Parrilla, mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Cuba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Bruno Rodriguez Parrilla, mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha