Makamu rais wa China na mwenzake wa Brazil waongoza mkutano wa COSBAN mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 07, 2024

Makamu Rais wa China Han Zheng akipeana mkono na Makamu Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Brazil Geraldo Alckmin mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

Makamu Rais wa China Han Zheng akipeana mkono na Makamu Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Brazil Geraldo Alckmin mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

BEIJING - Makamu Rais wa China Han Zheng amefanya mazungumzo na Makamu Rais wa Brazil Geraldo Alckmin na kuongoza kwa pamoja mkutano wa saba wa Kamati ya Uratibu na Ushirikiano wa Ngazi ya Juu ya China na Brazil (COSBAN) siku ya Alhamisi mjini Beijing.

Han amesema, chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, China na Brazil zimekuwa zikisaidiana kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi ya kila upande, na kuchukua ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote kama nguvu ya kujenga hamasa, kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa na kuimarisha uratibu wa kimkakati.

Amesema, ushirikiano katika sekta mbalimbali kama vile uchumi, biashara na anga ya juu umepata matokeo yaliyo dhahiri, akitoa mfano wa ushirikiano wa Kusini-Kusini.

China na Brazil ni nchi kubwa zinazoendelea na nchi wanachama muhimu wa BRICS ambazo zina maslahi mapana ya pamoja, Han amesema huku akiongeza kuwa China siku zote inafuatilia na kuendeleza uhusiano kati yake na Brazil na kutoa kipaumbele katika uhusiano wa kidiplomasia wa pande hizo mbili.

Han ametoa wito kwa pande zote mbili kuimarisha zaidi mawasiliano ya kimkakati na kuzidisha urafiki wa kunufaishana na ushirikiano wenye manufaa halisi.

Kwa upande wake Alckmin amesema uhusiano kati ya Brazil na China unavuka wigo wa pande mbili na una umuhimu wa kimkakati na ushawishi wa kimataifa na kwamba Brazil inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano na China na inapenda kuchukua maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi na maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa COSBAN kama mwanzo mpya ili kuimarisha zaidi mawasiliano na uratibu na China, na kuzidisha na kupanua mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, ili kuinua uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi mpya.

Han na Alckmin walisikiliza maoni mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wakuu wa idara husika za nchi hizo mbili kuhusu biashara, maendeleo ya viwanda ya aina mpya, uhusiano wa kisiasa, kilimo na ufugaji, sera za mambo ya fedha, miundombinu na mada nyinginezo.

Makamu Rais wa China Han Zheng na Makamu Rais wa Brazil Geraldo Alckmin wakitia saini waraka wa kumbukumbu wa mkutano wa saba wa Kamati ya Uratibu na Ushirikiano wa Ngazi ya Juu ya China na Brazil (COSBAN) mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

Makamu Rais wa China Han Zheng na Makamu Rais wa Brazil Geraldo Alckmin wakiongoza kwa pamoja mkutano wa saba wa Kamati ya Uratibu na Ushirikiano wa Ngazi ya Juu ya China na Brazil (COSBAN) mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

Makamu Rais wa China Han Zheng na mwenzake wa Brazil Geraldo Alckmin wakifanya mazungumzo mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

Makamu Rais wa China Han Zheng na mwenzake wa Brazil Geraldo Alckmin wakifanya mazungumzo mjini Beijing, China, Juni 6, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha