Jukwaa la kwanza la Ngazi ya Juu la Afrika kuhusu AI lafungwa kwa kutoa "Makubaliano ya Rabat"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 07, 2024

Picha iliyopigwa Juni 3, 2024 ikionyesha Jukwaa la Kwanza la Ngazi ya Juu la Afrika kuhusu Akili Mnemba(AI) katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mohammed VI cha Morocco huko Sale, Morocco. (Xinhua/Huo Jing)

Picha iliyopigwa Juni 3, 2024 ikionyesha Jukwaa la Kwanza la Ngazi ya Juu la Afrika kuhusu Akili Mnemba (AI) katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mohammed VI cha Morocco huko Sale, Morocco. (Xinhua/Huo Jing)

RABAT – Jukwaa la kwanza la ngazi ya juu la Afrika kuhusu Akili Mnemba (AI) lililoandaliwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mohammed VI cha Morocco na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), likiwa na kaulimbiu ya "Teknolojia ya AI: Nyenzo za Maendeleo Afrika." limefungwa siku ya Jumatano huko Sale, Kaskazini-Magharibi mwa Morocco, na kufikia "Makubaliano ya Rabat" kuhusu matumizi ya AI barani Afrika.

Wajumbe mbalimbali kutoka nchi na kanda zipatazo 30, zikiwemo nchi 15 za Afrika, walijadili hali ya sasa na matarajio ya teknolojia ya AI barani Afrika katika jukwaa hilo la siku tatu.

Wamesema kuwa Afrika haiwezi kukosa fursa zinazoletwa na AI, kwani ina mchango mkubwa katika kukuza usawa kwenye elimu , kuhifadhi utamaduni wa wenyeji wa Afrika, na kutimiza haki za wanawake wa Afrika.

Wakati huo huo, Afrika inahitaji kusawazisha msimamo wake na kutoa sauti yake yenyewe katika usimamizi wa Dunia wa teknolojia ya AI.

Wajumbe wameipitisha "Makubaliano ya Rabat" juu ya matumizi ya teknolojia ya AI barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kujitahidi kujenga mfumokazi wa pamoja wa kimataifa na jumuishi wa usimamizi wa AI; kuhimiza matumizi ya teknolojia ya AI katika idara za kiumma ili kuhudumia maslahi ya pamoja ya Afrika; kuhakikisha kwamba AI inahudumia kila mtu, na maendeleo yake yanapaswa kupatikana kwenye msingi wa kufuata maadili na vigezo vya haki za binadamu.

Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa UNESCO anayeshughulikia Mawasiliano na Habari Tawfik Jelassi, Mshauri wa Mfalme wa Morocco Andre Azoulay, na Waziri wa Vijana, Utamaduni na Mawasiliano wa Morocco Mohamed Mehdi BenSaid walihudhuria mkutano huo.

Mwanafunzi akitambulisha mradi wa kutumia teknolojia ya AI katika  ukarabati wa majengo kwenye Jukwaa la Kwanza la Ngazi ya Juu la Afrika kuhusu Akili Mnemba (AI) katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mohammed VI cha Morocco huko Sale, Morocco, Juni 4, 2024. (Xinhua/Huo Jing)

Mwanafunzi akitambulisha mradi wa kutumia teknolojia ya AI katika ukarabati wa majengo kwenye Jukwaa la Kwanza la Ngazi ya Juu la Afrika kuhusu Akili Mnemba (AI) katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mohammed VI cha Morocco huko Sale, Morocco, Juni 4, 2024. (Xinhua/Huo Jing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha