Mbio za Mashua ya dragon zaongoza msimu wa utalii wa Uganda na China nchini Uganda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 11, 2024

Wasanii wa Uganda na China wakichora kwa pamoja wakati mbio za mashua ya dragon zikifanyika kwenye Ziwa Victoria eneo la karibu na pwani la ziwa Victoria huko Entebbe, Uganda, Juni 9, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Wasanii wa Uganda na China wakichora kwa pamoja wakati mbio za mashua ya dragon zikifanyika kwenye eneo la karibu na pwani la ziwa Victoria huko Entebbe, Uganda, Juni 9, 2024. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

ENTEBBE -- Serikali ya Uganda na Ubalozi wa China nchini Uganda wameanzisha kwa pamoja msimu wa utalii wa nchi hizo mbili, na kuandaa mbio za mashua ya dragon kabla ya Siku ya jadi ya Duanwu ya China.

Kampuni za China nchini Uganda zilituma wapiga makasia bora, wa China na wa Uganda, kushiriki kwenye mbio hizo zilizofanyika siku ya Jumapili karibu na pwani ya Ziwa Victoria, katikati ya Uganda, ambazo pia zilivutia washiriki wenyeji.

Wataalamu wamesema tukio hilo linaonyesha kukua kwa uhusiano kati ya Uganda na China katika diplomasia, uchumi na utamaduni.

Waziri wa Utalii, Wanyamapori na Mabaki ya Kale wa Uganda, Martin Bahinduka, alikuwa mgeni mkuu. Aliwahimiza Waganda kujifunza kutoka kwa Wachina ambao wanathamini sana utamaduni wao, akisema Uganda ina urithi mkubwa wa kiutamaduni ambao unapaswa kuthaminiwa.

Waziri alisema Siku ya Duanwu ya mwaka huu ni jukwaa la kufahamisha watalii wa China kuhusu Uganda.

"Hili ni soko kubwa ambalo tunaweza kufaidika nalo," alisema Bahinduka. "Kuna Wachina 9,000 wanaokuja Uganda kila mwaka mpaka mwaka 2023. Tunaamini tunaweza kuongeza idadi hiyo hadi 15,000-20,000."

Fan Xuecheng, kaimu balozi wa China nchini Uganda, alisema kuandaa mbio za mashua ya dragon kutaimarisha msingi wa umma wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Uganda na kuhimiza zaidi mawasiliano ya kitamaduni kati ya nchi hizo mbili.

"Ingawa China na Uganda zina tamaduni tofauti, tuna dhana sawa ya kuunganisha historia, utamaduni na ustaarabu wa kisasa katika maendeleo ya utalii," alisema.

Siku ya Duanwu, ambayo ilikuwa Jumatatu, Juni 10 mwaka huu, huadhimishwa kila ifikapo siku ya tano ya mwezi wa tano wa kalenda ya kilimo ya China.

Timu ikishindana kwenye mbio za mashua ya dragon zilizofanyika eneo la karibu na pwani la Ziwa Victoria huko Entebbe, Uganda, Juni 9, 2024. (Photo by Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Timu ikishindana kwenye mbio za mashua ya dragon zilizofanyika eneo la karibu na pwani la Ziwa Victoria huko Entebbe, Uganda, Juni 9, 2024. (Photo by Hajarah Nalwadda/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha