Ndege ya Makamu wa Rais wa Malawi yapoteza mawasiliano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 11, 2024

Picha kutoka data iliyopigwa tarehe 9, Juni ikionesha makamu wa rais wa Malawi Saulos Chilima (kushoto) akishuka kutoka ndege baada ya kuwasili Lilongwe. (Picha ilichapishwa na Xinhua/Inatoka AP)

Picha kutoka data iliyopigwa tarehe 9, Juni ikionesha makamu wa rais wa Malawi Saulos Chilima (kushoto) akishuka kutoka ndege baada ya kuwasili Lilongwe. (Picha ilichapishwa na Xinhua/Inatoka AP)

Ofisi ya rais na baraza la mawaziri ya Malawi tarehe 10 ilitoa taarifa ikisema kuwa, ndege ya jeshi la ulinzi wa nchi aliyoipanda makamu wa rais wa Malawi Saulos Chilima asubuhi ya siku hiyo imepoteza mawasiliano, ndege hiyo ikibeba pia watu wengine tisa licha ya Chilima.

Taarifa hiyo ilisema, ndege hiyo iliyopoteza mawasiliano iliruka kutoka kwenye Lilongwe saa tatu na dakika 17 asubuhi kwa saa za Malawi, na kupangwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Mzuzu uliopo Kaskazini mwa nchi hiyo saa nne asubuhi hivi. Njiani ndege hiyo ilitoweka kwenye rada, na baada ya hapo mamlaka ya usafiri wa anga ilishindwa kuwasiliana na ndege hiyo.

Rais Lazarus Chakwera wa Malawi ametoa amri ya kuanzisha mara moja kazi ya uokoaji na kutafuta mahali ilipo ndege hiyo.

Habari zilisema kuwa, Chilima siku hiyo alikuwa amepanga kushiriki kwenye mazishi ya aliyekuwa waziri wa mambo ya mahakama wa nchi hiyo Ralph Kasambara.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha