Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Rwanda wang’ara katika shindano la lugha ya Kichina

(CRI Online) Juni 11, 2024

Shindano la "Daraja la Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya kigeni limefanyika Jumamosi katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Shindano hilo lililofanyika katika na Ubalozi wa China nchini Rwanda chini ya kaulimbiu "Dunia Moja, Falimia Moja," liliandaliwa na Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Rwanda, na lilihusisha umahiri wa kuongea Kichina na maonyesho ya vipaji.

Viateur Niyongabo, mwanafunzi kutoka Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu cha Rwanda aliibuka mshindi wa shindano hilo, na ataiwakilisha Rwanda katika fainali za mashindano hayo zitakazofanyika nchini China.

Akizungumza katika shindano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Elimu ya Msingi wa Rwanda Nelson Mbarushimana amesema, shindano hilo linaonyesha umuhimu wa mabadilishano ya elimu na utamaduni kati ya China na Rwanda.

Naye Balozi wa China nchini Rwanda Wang Xuekun ameipongeza Wizara ya Elimu ya Rwanda kwa kuunga mkono ufundishwaji wa lugha ya Kichina. Ameeleza matumaini yake kuwa vijana wa nchini Rwanda wataendelea kujifunza na kutumia vizuri lugha ya Kichina ili kutimiza ndoto zao na kutoa mchango katika maendeleo ya jamii na taifa lao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha