IGAD yaonya kuhusu majanga ya mafuriko ya ghafla katika Pembe ya Afrika

(CRI Online) Juni 11, 2024

Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) limetoa onyo juu ya mvua kubwa kupita kiasi katika maeneo mbalimbali ya Pembe ya Afrika, zitakazosababisha mafuriko na maporomoko ya udongo katika miezi ijayo.

Kituo cha Hali ya Hewa cha IGAD kimeonya katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu hali ya hewa kati ya mwezi Juni na Septemba mwaka huu, kuwa mvua kubwa kupita kiasi na hali ya joto kupita kiasi vinatabiriwa katika maeneo mengi ya Pembe ya Afrika.

Ripoti hiyo imesema, nchini Ethiopia, mafuriko ya ghafla yanaweza kutokea, maji kuongezeka katika mito na maziwa, na kusababisha maporomoko ya udongo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Nchini Kenya, ripoti hiyo imesema mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha mafuriko na maporomoko ya udongo, huku nchini Djibouti, mafuriko yanatarajiwa kutokea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kusababisha milipuko ya magonjwa ya wanyama na binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha