China yasonga mbele katika hatua ya kufuzu Kombe la Dunia kwa Asia licha ya kupoteza kwa Jamhuri ya Korea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 12, 2024

Son Heung-min (Kulia) wa Jamhuri ya Korea na Fang Hao wa China wakichuana kwenye mechi yao ya Kundi C ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa Nchi za Bara la Asia huko Seoul, Jamhuri ya Korea, Juni 11, 2024. (Xinhua/Yao Qilin)

Son Heung-min (Kulia) wa Jamhuri ya Korea na Fang Hao wa China wakichuana kwenye mechi yao ya Kundi C ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa Nchi za Bara la Asia huko Seoul, Jamhuri ya Korea, Juni 11, 2024. (Xinhua/Yao Qilin)

BEIJING - China imesonga mbele kichupuchupu kwenda raundi ya tatu ya mchujo wa kuwania kufuzu kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa nchi za Bara la Asia licha ya kushindwa na Jamhuri ya Korea 1-0 ugenini katika mchezo wa Kundi C uliochezwa Seoul, Jamhuri ya Korea, Jumanne usiku.

Baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Thailand nyumbani wiki iliyopita, China ilikuwa ikilazimika kuchukua angalau pointi moja katika mchezo wa mwisho wa raundi ya pili dhidi ya Jamhuri ya Korea ili kunusurika, vinginevyo bahati yao ingeamuliwa na matokeo ya mchezo kati ya Thailand na Singapore.

Hata hivyo, bao pekee la Lee Kang-in katika kipindi cha pili kwenye Uwanja wa Kombe la Dunia wa Seoul lilikatiza matumaini ya China ya kudhibiti hatma yao wenyewe. Ikianza mechi yake saa moja na nusu baadaye, Thailand imeweza kuishinda Singapore 3-1 nyumbani.

Matokeo hayo yameziacha China na Thailand zikiishia kuwa na pointi nane baada ya kushinda mechi mbili, kuambulia sare katika mechi mbili na kupoteza mechi mbili, pamoja na tofauti ya mabao sifuri na tisa ya kufunga. Lakini China imefanikiwa kusonga mbele nyuma ya kinara wa Kundi hilo la C, Jamhuri ya Korea ikiwa na rekodi bora ya ushindi wa mechi moja na sare katika mechi moja dhidi ya Thailand.

Droo ya raundi ya tatu ya kufuzu Kombe la Dunia kwa Nchi za Asia itafanyika Juni 27, ambapo timu 18 zitagawanywa katika makundi matatu, huku timu mbili za juu katika kila kundi zikipata nafasi za moja kwa moja kufuzu kwenye Kombe la Dunia lililopanuliwa la timu 48, wakati nafasi mbili zilizobaki zitaamuliwa katika raundi ya nne ya kufuzu kwa Kombe la Asia. 

Kipa Wang Dalei wa China akisalimia watazamaji baada ya mechi. (Xinhua/Yao Qilin)

Kipa Wang Dalei wa China akisalimia watazamaji baada ya mechi. (Xinhua/Yao Qilin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha