Mwanauchumi wa Pakistani: BRI ya China imeleta mabadiliko kwenye biashara ya kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 12, 2024

Moaaz Awan (kushoto) akifanya kazi kwenye Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Karot katika Jimbo la Punjab, Mashariki mwa Pakistan, Mei 2023. (Xinhua)

Moaaz Awan (kushoto) akifanya kazi kwenye Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Karot katika Jimbo la Punjab, Mashariki mwa Pakistan, Mei 2023. (Xinhua)

ISLAMABAD – Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) lililopendekezwa na China limeleta mabadiliko katika hali iliyopo na linaelekeza upya biashara ya kimataifa, Mohammad Zubair Khan, waziri wa zamani wa biashara wa Pakistan, ameliambia shirika la habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni akisema kuwa nchi nyingi zenye rasilimali bora hazikuweza kunufaika na rasilimali zao kutokana na kutounganishwa na nchi nyingine.

“Kwa upanuzi wa muunganisho wa BRI ambao ulipangwa na kuratibiwa na China, nadhani hilo litabadilika, na sote tutafaidika na muundo wa BRI,” amesema.

Akiangazia Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC), moja ya miradi kinara ya BRI, mwanauchumi huyo amesema inaunganisha Bahari ya Arabia na Ghuba ya Uajemi na Asia nzima iliyopo upande wa kaskazini.

Ikiwa ilizinduliwa Mwaka 2013, CPEC ni ukanda unaounganisha Bandari ya Gwadar katika Jimbo la Balochistan kusini magharibi mwa Pakistan na Mji wa Kashgar katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang wa China, ambao unaweka mkazo katika ushirikiano wa nishati, usafiri na viwanda katika awamu ya kwanza, huku awamu mpya ikipanuka katika nyanja za kilimo na shughuli za watu kujipatia kipato, miongoni mwa mengine.

Maendeleo ya Bandari ya Gwadar chini ya CPEC yatakuwa na mchango mkubwa katika kupunguza matatizo ambayo Pakistan imekuwa ikikabiliana nayo katika masuala ya biashara, muunganisho na ufikiaji wa masoko ya kimataifa, Khan amesema.

Picha hii iliyopigwa Mei 23, 2023 ikionyesha Eneo Maalum la Kiuchumi la Rashakai chini ya Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan katika Jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, kaskazini-magharibi mwa Pakistan. (Shirika la Barabara na Daraja la China/ Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Mei 23, 2023 ikionyesha Eneo Maalum la Kiuchumi la Rashakai chini ya Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan katika Jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, kaskazini-magharibi mwa Pakistan. (Shirika la Barabara na Daraja la China/ Xinhua)

Mwanauchumi huyo ambaye aliwakilisha Pakistan kwenye mkutano wa kwanza wa mawaziri wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), na ana uzoefu mkubwa wa kushirikiana na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), amepinga madai ya nchi za Magharibi kwamba mtindo wa uwekezaji wa BRI ni wa kinyonyaji na huzalisha mitego ya madeni kwa nchi mbalimbali.

"Mtindo wa nchi za Magharibi wa uwekezaji wa kigeni ni sawa na huo, kwa nini uwekezaji wa China uje kuwa madhara kwa nchi zinazoendelea? Hiyo sivyo," amesema, huku akibainisha kuwa dhana kwamba mradi wa CPEC umetengeneza mzigo wa madeni kwa Pakistan siyo sahihi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha