

Lugha Nyingine
China iko tayari kufanya juhudi endelevu kuongeza mabadilishano ya kitamaduni na maendeleo ya amani ya dunia
Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyopita umepitisha kwa kauli moja azimio lililopendekezwa na China la kuanzisha "Siku ya Kimataifa ya Mazungumzo kati ya Ustaarabu Mbalimbali" itakayoadhimishwa Juni 10 kila mwaka.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema, China iko tayari kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa kutekeleza kikamilifu azimio hilo na kufanya juhudi endelevu kuongeza maelewano na kufunzana kati ya ustaarabu mbalimbali na kuhimiza maendeleo ya amani duniani.
Bw. Lin pia amesema, hivi sasa, wakati mustakabali na hatma ya nchi zote ina uhusiano wa karibu, uvumilivu, kuishi pamoja, mabadilishano na kufunzana kati ya ustaarabu mbalimbali kunachukua nafasi isiyoweza kupuuzwa katika kuhimiza mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa jamii ya binadamu na kustawisha bustani ya ustaarabu wa dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma