Watu 86 wafariki baada boti kuzama katika tawi la Mto Kongo

(CRI Online) Juni 12, 2024

Watu 86 wakiwemo watoto 21 wamefariki baada ya boti kuzama katika Mto Kwa, moja ya matawi ya Mto Kongo, katika Jimbo la Mai-Ndombe, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano usiku kwa saa za huko karibu na kijiji cha Lediba, na kwamba boti hiyo ilikuwa inatoka mji wa Mushie kuelekea mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

Vyanzo vya habari pia vimesema watu 185 wameokolewa, na kuonya kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha