

Lugha Nyingine
Tanzania iko mbioni kutumia roboti katika utoaji wa huduma za Posta
Tanzania iko mbioni kuanza kutumia roboti katika utoaji wa huduma za vifurushi, wakati Umoja wa Posta Afrika (Papu) ukijipanga kuanzisha jukwaa la pamoja la biashara mtandao.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania, Merryprisca Mahundi, amesema hayo jana alipofungua mkutano wa 42 wa Baraza la wataalamu wa Umoja wa Posta Afrika kutoka nchi wanachama 45.
Wadau hao wamekutana mijini Arusha kujadili changamoto, utatuzi na fursa zilizopo katika uboreshaji wa huduma za posta katika nchi za Afrika.
Waziri Mahundi amesema wizara yake iko mbioni kufanikisha matumizi ya roboti katika utoaji wa huduma zake. Amesema katika kusaidia Shirika la Posta la Tanzania ili liendelee kukua na kutanuka kwa matumizi ya kidigitali, matumizi ya roboti yatakuwa suluhu ya kudumu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma