

Lugha Nyingine
China yatoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Makamu Rais wa Malawi
(CRI Online) Juni 13, 2024
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema siku ya Jumatano kwamba, China imetoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Makamu Rais wa Malawi Bw. Saulos Chilima na waathirika wengine wa ajali ya ndege iliyotokea Jumatatu wiki hii.
Bw. Lin amesema, katika wakati huu mgumu, serikali na watu wa China wanasimama kidete na serikali na watu wa Malawi, na anaamini kuwa, chini ya uongozi wa Rais Lazarus Chakwera, Malawi itaweza kuondokana na matatizo na kuondoka kwenye huzuni.
Kwenye hotuba yake aliyoitoa Jumanne, Rais Chakwera amesema ndege ya jeshi la nchi hiyo iliyokuwa imembeba Makamu Rais na watu wengine 9 ilianguka Jumatatu, na mabaki ya ndege hiyo yamepatikana, huku watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo wakiwa wamefariki.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma