

Lugha Nyingine
Ushuru wa EU kwa magari yanayotumia umeme ya China wapingwa na nchi nyingi za Ulaya
Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa tarehe 3 Juni 2024 ikionyesha kufuli kwenye minyororo mbele ya jengo la Kamati ya Umoja wa Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
BERLIN/BRUSSELS – Kamati ya Umoja wa Ulaya imetangaza siku ya Jumatano orodha ya ushuru wa forodha wa kujilinda kibiashara ambao utaweka ushuru kwa magari yanayotumia umeme ya betri (EVs) kutoka China, ikisababisha upingaji na wasiwasi kutoka kwa serikali na kampuni za nchi mbalimbali barani Ulaya.
Ushuru huo wa muda unaotakiwa kutozwa na Kamati ya Umoja wa Ulaya kwa magari hayo kutoka China unaanzia asilimia 17.4 hadi asilimia 38.1.
Waziri wa Uchumi wa Kitaifa wa Hungary Marton Nagy amelaani hatua hiyo akisema ni ya kujilinda kibiashara kupita kiasi. Amesema katika taarifa yake kwamba "kujilinda kibiashara siyo suluhu," na uamuzi wa Kamati ya Umoja wa Ulaya utabagua isivyo haki wazalishaji bidhaa wa China na kuvuruga ushindani wa soko, ambao umekuwa muhimu kwa Umoja wa Ulaya (EU).
Volker Wissing, waziri wa Mambo ya Kidijitali na Uchukuzi wa Ujerumani, amesema ushuru utaathiri kampuni za Ujerumani na mauzo yao nje. "Magari lazima yawe ya bei nafuu kupitia ushindani zaidi, masoko ya wazi na hali bora zaidi ya eneo katika EU, siyo kupitia vita vya biashara na kujitenga kimasoko," ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.
Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa tarehe 6 Juni 2024 ikionyesha gari linalotumia umeme kwenye kituo cha kuchajia karibu na jengo la Kamisheni ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)
Mkurugenzi Mtendaji wa BMW Oliver Zipse amekosoa mpango huo wa Kamati ya Umoja wa Ulaya kwa kuuelezea kuwa ni "njia mbaya ya kufuata," akisema kuwa utaharibu kampuni na maslahi ya Ulaya. "Kujihami kibishara kunahatarisha kupanuka zaidi: Ushuru husababisha ushuru mpya, hadi kutengana kibiashara badala ya ushirikiano," amesema.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Stellantis, Carlos Tavares (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Leapmotor, Zhu Jiangming wakishikana mikono kwenye Hafla ya Kusaini Makubaliano ya Ushirikiano wa Kimkakati wa Stellantis na Leapmotor mjini Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Oktoba 26, 2023. (Stellantis/ Xinhua)
Serikali ya Sweden inataka kujua kama Kamati ya Umoja wa Ulaya imetumia kikamilifu njia zingine tofauti na ushuru, Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na Biashara ya Nje wa Sweden Johan Forssell amesema. "Kwa ujumla tuna mashaka na ushuru. Mtu fulani anapaswa kuulipa, na katika suala hili, mapema au baadaye, atakuwa ni mnunuzi wa kulipa," shirika la habari la Sweden, TT limemnukuu Forssell akisema.
Magari ya NIO yakionyeshwa kwenye Jengo la NIO huko Oslo, mji mkuu wa Norway, Septemba 30, 2021. (Xinhua/Zhu Sheng)
Ikiwa ni nchi isiyo mwanachama wa EU, Norway imesema haitafuata EU kuongeza ushuru kwa magari yanayotumia umeme ya China. Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Trygve Slagsvold Vedum ametangaza uamuzi huo siku ya Jumatano.
"Kutoza ushuru kwa magari ya China siyo muhimu wala haifai kwa serikali hii," shirika la kitaifa la utangazaji la Norway NRK limemnukuu Vedum akisema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma