

Lugha Nyingine
Malawi yatangaza siku 21 za kuomboleza kifo cha Makamu Rais Chilima
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera (Kushoto) akisubiri kuwasili kwa helikopta iliyobeba miili ya Makamu Rais Saulos Chilima na waathiriwa wengine kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mjini Lilongwe, Malawi, Juni 11, 2024. (Picha na Roy Nkosi/Xinhua)
LILONGWE - Malawi imetangaza kipindi cha siku 21 cha kuomboleza kifo cha Makamu Rais Saulos Chilima, ambaye amefariki katika ajali ya ndege iliyotokea siku ya Jumatatu pamoja na wengine wanane waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Waziri wa Habari na Mambo ya Kidijitali Moses Kunkuyu ametoa tangazo hilo siku ya Jumanne, akiongeza kuwa mwili wa Makamu wa Rais utapewa mazishi ya hadhi ya kiserikali.
Kamati maalum inayoongozwa na Waziri wa Mambo ya Mahakama Titus Mvalo itaratibu mipango ya mazishi ya makamu rais huyo, amesema waziri huyo.
Hali ya huzuni imeikumba nchi hiyo huku bendera ya taifa la nchi hiyo na bendera zingine zote za kitaasisi zikipeperuka nusu mlingoti.
Chilima na wasaidizi wake, pamoja na mke wa rais wa zamani Patricia Shanil Dzimbiri, walikuwa njiani kuelekea kwenye mazishi ya Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Mahakama Ralph Kasambara, na ajali hiyo ilitokea kwa sababu ya hali mbaya ya hewa, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka.
Helikopta iliyobeba miili ya Makamu Rais Saulos Chilima na waathiriwa wengine ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mjini Lilongwe, Malawi, Juni 11, 2024. (Picha na Roy Nkosi/Xinhua)
Ambulesi iliyobeba mwili wa Makamu Rais Saulos Chilima ikionekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mjini Lilongwe, Malawi, Juni 11, 2024. (Picha na Roy Nkosi/Xinhua)
Mary Chilima (Kati), mke wa Makamu Rais wa Malawi Saulos Chilima akisubiri kuwasili kwa helikopta iliyobeba miili ya Chilima na waathiriwa wengine kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mjini Lilongwe, Malawi, Juni 11, 2024. (Picha na Roy Nkosi/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma