Nchi za Afrika Mashariki zazindua mfumo wa mwongozo wa kutokomeza ugonjwa wa usubi

(CRI Online) Juni 13, 2024

Nchi za Afrika Mashariki zimezindua mfumo wa pande zote utakaoongoza wadau wa sekta ya afya katika kutokomeza ugonjwa wa usubi.

Taasisi ya utafiti ya Dawa na Magonjwa Yasiyopewa umuhimu (DSDi) imesema katika taarifa yake iliyotolewa jijini Nairobi, Kenya, kwamba eneo la Afrika Mashariki lilichukua asilimia 70 ya visa vya wagonjwa wa usubi duniani mwaka 2022, na nusu ya visa hivyo viliwakuta watoto wenye umri wa chini ya miaka 15.

Ugonjwa huo ambao haujapewa kipaumbele kinachotakiwa kama moja ya magonjwa ya kitropiki unasababishwa na vimelea na dalili zake ni pamoja na homa, kupungua uzito, kupanuka kwa ini na bandama.

Mwongozo huo umeandaliwa na Shirika la Afya Duniani na washirika wake ikiwemo Taasisi ya DNDi na mawaziri wa afya katika kanda hiyo, na umetoa maeneo matano ya kimkakati, ambayo ni pamoja na kutambua mapema na kutibu ugonjwa huo, kutoa elimu, na utafiti.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha