

Lugha Nyingine
Umoja wa Mataifa wapeleka walinzi wa amani kulinda raia mashariki mwa DRC
(CRI Online) Juni 13, 2024
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamepelekwa kulinda raia dhidi ya mapigano kati ya makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo.
Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema siku ya Jumatano kuwa, wafuasi wa makundi ya Zaire na CODECO wamepigana katika eneo la machimbo ya madini lililoko umbali wa kilomita 40 kutoka mji wa Bunia, Jimbo la Ituri, hivyo walinzi wa amani wa Umoja huo wamepelekwa ili kulinda raia.
Amesema tangu tarehe 25 Mei, kundi la ADF limekuwa likifanya mashambulio mfululizo katika Majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma