Mkutano wa kilele wa G7 wafunguliwa huku kukiwa na maandamano ya kupinga

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 14, 2024

Viongozi wa G7 wakiwa katika picha ya pamoja na warukaji angani na maparachuti waliobeba bendera za mataifa huko Borgo Egnazia, karibu na mji wa Fasano katika Mkoa wa Apulia, Italia, tarehe 13 Juni 2024. (Xinhua/Li Jing)

Viongozi wa G7 wakiwa katika picha ya pamoja na watumbuizaji wa urukaji angani na maparachuti waliobeba bendera za mataifa huko Borgo Egnazia, karibu na mji wa Fasano katika Mkoa wa Apulia, Italia, tarehe 13 Juni 2024. (Xinhua/Li Jing)

FASANO, Italia - Mkutano wa kilele wa siku tatu wa Kundi la Nchi Saba (G7) Mwaka 2024 umeanza siku ya Alhamisi huko Borgo Egnazia, sehemu ya mapumziko karibu na Mji wa Fasano katika Mkoa wa Apulia, Kusini mwa Italia, huku kukiwa na maandamano ya kupinga ambapo migogoro ya Ukraine na Mashariki ya Kati na uhusiano na Nchi za Kusini vinaongoza ajenda ya mkutano huo.

Usimamizi wa Teknolojia za Akili Mnemba (AI), masuala yanayoikabili Afrika na mabadiliko ya tabianchi pia yamejumuishwa katika vikao muhimu.

Italia inashikilia urais wa zamu wa G7 mwaka huu. Mbali na viongozi wa G7, wakuu wa nchi zaidi ya kumi na wa mashirika ya kimataifa wamealikwa kuhudhuria mkutano huo.

Katika siku ya kwanza, kundi hilo limejadili rasimu ya mpango wa mkopo wa dola bilioni 50 za Marekani kwa Ukraine, kwa kutumia mali zilizozuiliwa za Russia kama dhamana.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Maria Zakharova Alhamisi alijibu kuwa, mipango ya G7 haitazinufaisha nchi za Magharibi na huenda ikasababisha msukosuko mpya wa kiuchumi.

Marekani na Japan kila moja imetia saini mikataba ya usalama na Ukraine, hali ambayo imezifanya kuwa nchi wanachama wawili wa mwisho wa G7 zilizotia saini mikataba hiyo.

Maandamano ya kupinga mkutano huo wa G7 yanafanyika katika maeneo mengi karibu na eneo la mkutano huo.

Katika siku ya ufunguzi, huko Brindisi, mji ulio umbali wa kilomita 60 kutoka eneo la mkutano huo, waandamanaji walishikilia bendera za Palestina na kuonyesha mabango yenye kauli mbiu kama vile "Susia G7," "Acha Kuharibu Sayari," na "Hapana Vita Zaidi." Wameikosoa G7 kwa kushindwa kutoa mchango mzuri katika ulinzi wa mazingira, haki ya kijamii na kudumisha amani.

Kundi la G7 linajumuisha Canada, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Japan. 

Viongozi wa G7 wakiwa katika picha ya pamoja na warukaji angani na maparachuti waliobeba bendera za mataifa huko Borgo Egnazia, karibu na mji wa Fasano katika Mkoa wa Apulia, Italia, tarehe 13 Juni 2024. (Xinhua/Li Jing)

Viongozi wa G7 wakiwa katika picha ya pamoja na watumbuizaji wa urukaji angani na maparachuti waliobeba bendera za mataifa huko Borgo Egnazia, karibu na mji wa Fasano katika Mkoa wa Apulia, Italia, tarehe 13 Juni 2024. (Xinhua/Li Jing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha