

Lugha Nyingine
China na New Zealand zaahidi kupanua wigo wa biashara na kuzidisha mawasiliano kati ya watu
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon mjini Wellington, New Zealand, Juni 13, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)
WELLINGTON - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon siku ya Alhamisi mjini Wellington, wakikubaliana kupanua wigo wa biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili na kuongeza mawasiliano kati ya watu. Wakati wa mazungumzo yao, Li amesema ziara yake inafanyika wakati wa maadhimisho ya miaka 10 tangu Rais Xi Jinping afanye ziara rasmi nchini New Zealand na kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo.
Katika miaka hiyo 10 iliyopita, haijalishi jinsi mazingira ya kimataifa yanavyobadilika, China na New Zealand zimekuwa zikishikilia kuheshimiana, kuwa na ujumuishaji, kufanya ushirikiano na kupata maendeleo kwa pamoja, kuhimiza uhusiano wa pande mbili kupata maendeleo makubwa, na kufanya mafanikio mengi "ya kwanza" katika ushirikiano wa pande mbili, amesema.
Li amesema, China ingependa kufanya juhudi pamoja na New Zealand katika kuendeleza urafiki wao wa jadi, kuenzi moyo wa "kujitahidi kuwa wa kwanza," ili kuchochea ukuaji wa uchumi, na kufanya jitihada za kuendeleza kwenye ngazi ya juu uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na New Zealand ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wao.
China ingependa kufanya juhudi pamoja na New Zealand katika kupanua biashara siku hadi siku, kutafuta nguvu za kifursa za ushirikiano katika sekta za uchumi wa kidijitali, uchumi wa kijani, magari yanayotumia nishati mpya na viwanda vyenye uvumbuzi, na kuhimiza kwa pamoja ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda, amesema Waziri Mkuu wa China.
Pia ametoa wito kwa New Zealand na China kuondoa usumbufu usio wa kiuchumi katika uhusiano wao wa kiuchumi na kibiashara ili kuwapa wafanyabiashara matarajio na mazingira mazuri ya biashara, akiongeza kuwa China inakaribisha uwekezaji zaidi kutoka kampuni za New Zealand.
Kwa upande wake Luxon amesema katika miaka 10 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, New Zealand na China zimeshuhudia maendeleo makubwa katika uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na mawasiliano ya karibu kati ya watu, na kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.
Amesema New Zealand inafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja na ingependa kuimarisha mazungumzo na mawasiliano kwenye ngazi ya juu na China, kuzidisha zaidi ushirikiano katika kilimo, chakula, viwanda vyenye Uvumbuzi na ulinzi wa mazingira, kuongeza mawasiliano ya kiutamaduni na kusukuma maendeleo endelevu na ya pande zote uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Nchi hizo mbili zimekubaliana kuanzisha mazungumzo kuhusu orodha hasi ya biashara ya huduma. Baada ya mkutano huo, Li na Luxon walishuhudia utiaji saini nyaraka za ushirikiano wa pande mbili kuhusu biashara ya huduma, mazingira ya biashara, na sayansi na teknolojia.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa New Zealand Christopher Luxon mjini Wellington, New Zealand, Juni 13, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma