

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu Li: Ushirikiano wa China na Australia unaweza kuvuka Pasifiki, kuzipita tofauti
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akitembelea bustani ya wanyama ya Adelaide kwa ajili ya ushirikiano kati ya China na Australia kuhusu ulinzi na utafiti wa panda mjini Adelaide, Australia Juni 16, 2024. (Xinhua/Li Tao)
ADELAIDE, Australia - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema siku ya Jumapili kwamba kama pande zote mbili zinauthamini, ushirikiano kati ya China na Australia utaweza kuvuka Bahari kubwa ya Pasifiki, kuzipita tofauti, na kufikia mafanikio na maendeleo kwa pamoja na kupata matokeo yenye manufaa kwa pande zote mbili.
Ameyasema hayo alipotembelea bustani ya wanyama ya Adelaide kwa ajili ya ushirikiano kati ya China na Australia kuhusu ulinzi na utafiti wa panda, akiambatana na Gavana wa Australia ya Kusini, Frances Adamson, Waziri Mkuu wa Australia ya Kusini Peter Malinauskas, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong na Waziri wa Biashara na Utalii wa Australia Don Farrell. Bustani ya Wanyama ya Adelaide ndiyo bustani pekee ya wanyama ya Australia inayohifadhi panda.
Akiwa kwenye Banda la Panda katika bustani hiyo, Li alisikia ripoti za wataalam wa China na Australia kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kuhusu utafiti juu ya uhifadhi wa panda pamoja na kuzaliana na kutunzwa kwa panda nchini Australia.
Li amesema kwamba jozi pekee ya panda katika Dunia ya Kusini, Wang Wang na Fu Ni, sasa wanaishi katika bustani hiyo ya Adelaide, anafurahi kuona kwamba ingawa Wang Wang na Fu Ni wako mbali na nchi yao, wametunzwa vizuri na kuishi maisha ya utulivu na furaha nchini Australia. Amesema wamekuwa wajumbe wa urafiki kati ya China na Australia, na ni ishara ya urafiki mkubwa kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Li amesema kuwa Wang Wang na Fu Ni watarejea China mwaka huu kama ilivyokubaliwa na pande hizo mbili, na China ingependa kuendelea na ushirikiano na Australia katika ulinzi na utafiti wa panda, na anatumai kuwa Australia daima itakuwa makazi rafiki kwa panda.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akizungumza na wanafunzi wenyeji wakati akitembelea bustani ya wanyama ya Adelaide kwa ajili ya ushirikiano kati ya China na Australia kuhusu ulinzi na utafiti wa panda mjini Adelaide, Australia Juni 16, 2024. (Xinhua/Li Tao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma