Wachumi nchini Tanzania wapongeza marufuku ya matumizi ya fedha za kigeni katika shughuli za ndani

(CRI Online) Juni 17, 2024

Wachumi na wachambuzi wa masuala ya biashara nchini Tanzania wamepongeza azma ya serikali ya kuhakikisha kuwa fedha za kigeni hazitumiwi kununua au kulipia bidhaa na huduma za ndani ya nchi hiyo, wakibainisha kuwa hatua hiyo itachangia kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Hayo yamejiri baada ya Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba kuagiza wadau wote wanaohusika, kama vile taasisi za umma, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa na wananchi wote waliokuwa wakitoa bei za bidhaa na huduma kwa fedha za kigeni kuacha ifikapo mwezi ujao na kuhakikisha bei zinanukuliwa na kulipwa kwa shilingi ya Tanzania.

Katika mahojiano tofauti na gazeti la Serikali ya Tanzania la Daily News, wachumi hao wamesema kukataza kulipia au kununua bidhaa na huduma za ndani kwa fedha za kigeni si tu kutashughulikia changamoto ya uhaba wa dola za Marekani bali pia kuimarisha uchumi wa nchi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha