

Lugha Nyingine
Rais wa Namibia atoa wito wa dhamira ya elimu bora barani Afrika
(CRI Online) Juni 17, 2024
Rais Nangolo Mbumba wa Namibia ametoa wito wa kuhakikisha elimu bora inapatikana barani Afrika, akisema Bara la Afrika litanufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwekeza katika elimu na vijana, kama ilivyoainishwa kwenye Ajenda ya Afrika kuelekea mwaka 2063.
Rais Mbumba aliungana na wanamibia na bara zima la Afrika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika, akisisitiza umuhimu wa siku hiyo kwa kukumbuka ujasiri wa vijana wa Afrika Kusini ambao walipinga mfumo wa kibaguzi wa elimu.
Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ya "Elimu kwa watoto wote barani Afrika: wakati ni sasa", Rais Mbumba amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma