Miitikio ya dharura yawekwa katika kiwango cha juu huku mvua kubwa ikinyesha kusini mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 18, 2024

Picha iliyopigwa Juni 16, 2024 ikionyesha hali ya mafuriko huko Wuyishan  ya Mji wa Nanping, Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China. (Xinhua/Jiang Kehong)

Picha iliyopigwa Juni 16, 2024 ikionyesha hali ya mafuriko huko Wuyishan ya Mji wa Nanping, Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China. (Xinhua/Jiang Kehong)

BEIJING - Mikoa kadhaa ya China imeanzisha au kupandisha viwango vya miitikio yao ya dharura kwa kukabiliana na mafuriko baada ya kukumbwa na mvua kubwa na kupanda juu kwa viwango vya maji ya mito ambapo hadi kufikia sasa, mvua kubwa imesababisha uharibifu mbaya katika Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China na Mkoa wa Guizhou, Kusini Magharibi mwa China.

Watu wanne wameuawa, na wengine wawili hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kukumba Wilaya ya Wuping mkoani Fujian, taarifa ya serikali ya eneo hilo iliyotolewa Jumatatu imesema.

Kati ya Jumapili na Jumatatu alasiri, watu karibu 47,800 huko Wuping, katika Mji wa Longyan, walikuwa meathiriwa na mvua. Kipimo cha juu zaidi cha mvua katika kipindi cha saa 24 zilizopita huko Wuping kilikuwa milimita 372.4.

Makao makuu ya idara ya kudhibiti mafuriko na misaada ya unafuu wa ukame huko Wuping yameanzisha mwitikio wa dharura wa Kiwango cha I kwa mvua kubwa. China ina mfumo wa mwitikio wa dharura wa kudhibiti mafuriko wa ngazi nne, huku Kiwango cha I kikiwa kikali zaidi.

Mkoani Guizhou, vituo 113 vya ufuatiliaji wa hali ya hewa katika tarafa 29 (miji na wilaya) vilikuwa vikishuhudia mvua kubwa kuanzia Jumapili hadi Jumatatu, huku mvua ya juu ikizidi milimita 200.

Makao makuu ya udhibiti wa mafuriko na misaada ya unafuu wa ukame ya Mkoa wa Hunan katikati mwa China na Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China pia yamepandisha viiwango vya mwitikio wa dharura kwa Ngazi ya IV kwa mafuriko.

Mashirika ya reli yamesitisha huduma 85 za treni kupitia Hunan kuanzia Jumatatu hadi Juni 20 kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la magharibi mwa jimbo hilo.

Zaidi ya hayo, Mkoa wa Guangdong na Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China pia imepandisha viwango vya miitikio yao ya dharura ya kudhibiti mafuriko. Hadi ilipofika saa 8 mchana Jumatatu, vituo 19 vya upimaji viwango vya maji vya mito huko vilikuwa vimerekodi viwango vya maji juu ya kiwango cha tahadhari, idara ya rasilimali ya maji ya mkoa huo imesema.

Wizara ya Rasilimali za Maji ya China na Idara ya Hali ya Hewa ya China pia zimedumisha kwa pamoja tahadhari ya juu zaidi ya mvua za milimani siku hiyo hiyo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha