Waziri Mkuu wa China asisitiza kudumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo thabiti ya uhusiano kati ya China na Australia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 18, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese wakifanya Mkutano wa tisa wa Mwaka wa Viongozi wa China na Australia mjini Canberra, Australia, Juni 17, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

CANBERRA - Siku ya Jumatatu asubuhi, kwenye ziara yake rasmi nchini Australia, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesisitiza umuhimu wa kudumisha na kuendeleza mwelekeo mzuri wa uhusiano kati ya pande hizo mbili.

Kwa mujibu wa wataalamu, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa na misukosuko katika muongo mmoja uliopita, hali ambayo, kwa bahati nzuri, imerejeshwa tena kwenye njia sahihi hatua kwa hatua kupitia juhudi za pamoja na majadiliano ya ngazi ya juu.

Wamesema, ingawa zinatenganishwa na bahari, China na Australia kwa muda mrefu zimekuwa zikisonga mbele bega kwa bega katika historia, zikinufaika sana na ushirikiano wa kunufaishana.

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu Rais Xi Jinping wa China afanye ziara ya kiserikali nchini Australia na kuanzisha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Australia.

Sifa muhimu za uhusiano kati ya China na Australia ni ushirikiano wa kunufaishana, na maendeleo ya China na Australia ni fursa badala ya kuwa changamoto kati yao, Waziri Mkuu Li amesema kwenye Mkutano wa tisa wa Mwaka wa Viongozi wa China na Australia na Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese.

Akizungumzia uhusiano wa pande mbili katika muongo mmoja uliopita, Li amesema kuwa uzoefu muhimu zaidi na msukumo ni kushikilia kuheshimiana na ushirikiano wa kunufaishana, na kutafuta maelewano ya pamoja huku kukiwa na kuzuia tofauti.

Li pia amesema kwenye mkutano wake na Albanese kwamba China inapenda kushirikiana na Australia ili kujenga ushirikiano wa kimkakati uliokomaa, thabiti na wenye matunda zaidi kati ya China na Australia ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

Ziara ya Waziri Mkuu wa China imeangalia matarajio ya maendeleo ya siku zijazo, amesema Guo Shengxiang, mkurugenzi wa Taasisi ya Uvumbuzi ya Mambo ya Fedha na Teknolojia ya Australia. "Ziara ya Waziri Mkuu Li imeleta matumaini katika dunia inayobadilika," Guo amesema.

Li yuko katika ziara ya nchi tatu kuanzia Juni 13 hadi 20. Mbali na Australia, amefanya ziara rasmi nchini New Zealand na Malaysia.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese wakifanya Mkutano wa tisa wa Mwaka wa Viongozi wa China na Australia mjini Canberra, Australia, Juni 17, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese wakifanya Mkutano wa tisa wa Mwaka wa Viongozi wa China na Australia mjini Canberra, Australia, Juni 17, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha